Habari mkuu wa Libeneke la Globu ya Jamii.

Tafadhali nakuomba ufikishea ujumbe kwa wahusika ili watanzania wenzetu waliokwama kwenye Basi la Kampala coach huko Eldoret nchini Kenya lililokuwa likitokea Uganda,watanzania hawa walitegemea kufika leo jijini Dar kutokea Uganda.

Basi limekuwa na matataizo tangu likitoka Kampala jana mida ya saa kumi jioni na limekuwa likihalibika mara kwa mara na kuwapa wakati mgumu abiria na hawajapata ushirikiano wowote toka kwa wamiliki wa mabasi mpaka hivi sasa.

 wamekwama nchini Kenya maeneo ya Eldoret na hawana fedha Ya chakula,please nakuomba ufikishe ujumbe kwa wahusika ili waweze kusaidiwa maana wamesharipoti Police Kenya lakini hawajasaidiwa wanasema iko juu ya uwezo wao.

kuna watu wapo huko unaweza kuwapata kwa simu namba hii 0754 66 17 80 

 Aksante kwa ushirkiano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. JK alitaka ajenge barabara kupitia Serengeti mkampinga eti wanyama watauawa, sasa ndo muone mawazo yake yalikuwa mazuri kwenu. Barabara inaweza kujengwa na wanyama wasigongwe kama ubunifu katika kujenga barabara hiyo utazingatiwa.

    ReplyDelete
  2. Hao wakenya wanakataa kuwasaidia Watanzania, mbona wao tunawapa ushirikiano mkubwa wanapopata matatizo wakiwa Tanzania???..Hawakumbuki ile ajali ya mwezi Mei huko Wami tuliwasaidia sana??? Acheni roho mbaya Police wa Kenya, najua ninyi kwa rushwa ndo balaa! Hebu saidieni jirani zenu huko!

    ReplyDelete
  3. mabasi ya kampala Coach yamechoka sana! ni lini itaibuka tena kampuni ya tanzania kama scandinavia express?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...