Wachezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ya Serengeti Boys wakishangilia bao lililofungwa na Mudathiri Yahaya Abbas wakati timu hiyo ilipopambana na Congo Brazzaville katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa vijana wenye umri huo, zitakazofanyika  mwakani nchini Morocco. Serengeti Boys imeshinda 1-0.
 Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Jacob Michelsen na msaidizi wake Jamhuru Kihwelo  wakipongezana baada ya mchezo kumalizika. 
  Mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ya Serengeti Boys, Hussein Twaha akiwatoka mabeki wa timu ya Congo Brazzaville katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za Afrika kwa vijana wenye umri huo zitakazofanyika  mwakani nchini Morocco. Mchezo huo ulifanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Serengeti Boys imeshinda 1-0. 
 Mshambuliaji wa timu ya Srengeti Boys, Faridi Mussa (katikati) akiwania mpira huku beki wa Cpngo Brazzaville, Tmouele Ngampio akijaribu kumzuia. Kulia ni Golipika wa Congo Brazzaville, Ombandza Mpea akijaribu kuokoa hatario langoni mwake. 
 Waamuzi wa mchezo huo wakitoka baada ya kwisha kwa pambano hilo
 Mshambuliaji wa Serengeti Boys, Tumain Baraka akichuana na beki wa Congo Brazzaville, Okombi Francis
 Heka heka katika lango la Congo Brazzaville
Selemani Hamis Bofu  akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Congo Brazzaville, Tmouele Ngampio.Picha na Habari Mseto Blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kwanza hongereni makocha licha ya kufanya kazi ktk mazingira magumu, pili wachezaji kwa kuweka mbele heshima ya taifa. Kocha jamuhuri kihwelo jana ktk gazeti fulani alilalamikia viongozi wa serikali kwa kutosapoti timu na akasema kwanza wasisubiri washinde ndio waanze kujisogeza yale maneno yamenichoma sana kama raia na mzalendo, ningependa ushindi huu utumike kuwavuta viongozi wa serikali kuisapoti timu maana mbele ni kuzito zaidi licha ya maneno ya ukweli ya kocha kihwelo na watambue kwamba ni wajibu wao kufanya hivyo kama viongozi. Umoja ni nguvu tanazania mbele mbele mbele zaidi.

    ReplyDelete
  2. Hongereni sana vijana,kazi bado sana.Nafasi muhimu sanba ya kwenda kuonekana kwenye 'kioo'na kupata timu kubwa za kuchezea baadae.

    ReplyDelete
  3. hongera kwa kushinda, lakini timu yetu ni dhaifu sana, wachezaji wazito kama wamefungiwa mawe miguuni, hawana pumzi(stamina), wako taratibu sana, wanapoteza muda bila sababu, muda mwingi akili zao hazipo mchezoni, wanacheza kama wapo mtaani(chandimu) kwamba muda wowote wataitwa na wazazi wao kwenda kula, makocha pengine wameweza kuwafundisha kucheza mpira lakini hawajafanikiwa kuwaelewesha wajibu waliopewa na taifa

    ReplyDelete
  4. Mimi nawapongeza vijana wamecheza ipasavyo na kushinda nina imani kuwa watashinda mechi ya marudiano au kuhakikisha kuwa Wacongo hawafungi goli hata moja. Mimi nawashangaa sana baadhi ya Watanzania hasa waandishi wa habari kila wakati ni kuyabeza mafanikio, utawasikia tumeshinda halafu lakini....lakini.... . lakini zinakuwa nyingi sana. Lazima Watanzania tujivunie mafanikio yetu na tuachane na inferiority complex kuwa hatuwezi na kuwa ushindi ni mdogo au umepatikana kwa bahati. Kama timu pinzani ni boroa mbona imefungwa? Ushindi wa goli 1 kwa 0 mchezoni ni mkubwa sana kama vijana wa Serengeti wameweza kugusa nyavu za wapinzani wao na wapinzani kushindwa kuziona nyavu za vijana wa Serengeti kwa dakika zote 90 hayo kwangu mimi ni mafanikio makubwa, haifai kuwabeza vijana ambao wamepambana na timu inayosemekana ina vijeba na ambayo wengi wa wachezaji wake walishacheza fainali kama hizo zilizotangulia na sijui wakati huo walikuwa na umri gani? Inabidi kuthamini ushindi tuliopata na kuwapa moyo Serengeti Boys wawe na ujasiri na ari ya ushindi, nchi za wenzetu ndivyo wafanyavyo.

    JohnJohn

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...