Kwanza nakusalimu, na kukupa pole kwa majukumu yako yakila siku.
Naomba uniwekee haya malalamiko yangu kwenye Blog yako, hapa Arusha eneo la Fire kuna ujenzi wa barabara unaoendelea zaidi ya mwezi sasa sikatai maendeleo ya mji wetu hasa tukizunguzia kwasasa ni jiji, kero yangu hapa ni pale wachina walivyofukua mabomba na kuyakata kitendo hicho kimetusababishia matatizo ya maji hadi hivi leo yapata mwezi mmoja na nusu hatujapata maji,
tumejaribu kuwasiliana na watu wa Idara ya Maji wana majibu ya ghafla kwamba tunataarifa ya tatizo lenu tunalifanyia kazi, huweze kuamini hakuna kilichoendelea hadi leo hao mafundi wa Idara ya Maji hawajajigusa.
Nilikuwa naomba huyo Engineer wa maji ashughulike swala hili mana tunateseka hatuna mahali pa kupata maji na sababu halisi hatuijui.
Mwisho nasisitiza kuwa wahusika walishughulikie mapema kabla hali haijawa mbaya, wanasema mteja ni mfalume mbona sisi ni wateja wao lakini hawatujali.
Ni mimi mwana jamii katika mateso
Arusha


Arusha Mjini mmeyakanyaga mawaya wenyewe kwa kuwapa Dhamana Wabunge wa Vyama Pinzani na wenye Siasa za Kisanii.
ReplyDeleteArusha 'ilikuwa' Geneva ya Africa kwa uzuri na usafi na sio kwa sababu Mahakama ya Mauaji ya Rwanda ICTR kuwepo hapo, na ndio maana Makao Makuu ya Afrika ya Mashariki yakapendekezwa kuwepo hapo.
Mlipokuwa na Mbunge wa CCM shida kama hii ilikuwepo?
Mlipokuwa na Mbunge wa CCM Mji hadhi yake ilikuwa chini kama ilivyo sasa?
Ni kwa nini mumtafute Mchawi wa kukosa maji wakati wenyewe mmeyataka?
Maji hakuna eeeeh?
ReplyDeleteWaambieni OPERESHENI SANGARA au ile M4C WAKATE PANGA LA PESA WALIZOCHANGISHA WALETE MAJI ARUSHA!
Kama hakuna maji mwambieni Mbunge wenu wa zamani Godbles Lema awape maji!
ReplyDeleteHapa ndio pa kuonyesha uzalendo wake ya kuwa bado yupo na ninyi!!!
Sasa kutolewa Ubunge na ndio uwana Arusha amenyang'anywa pia?
Si mlilia chai wenyewe iweje sasa mnalalamika mnaungua?
ReplyDeleteHiyo ndio joto ya jiwe ya kuutaka Upinzani!!!
Mtakunywa maji ya mitaro na mifereji kwa kuchagua Upinzani!
ReplyDelete