Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Bw. Samson Chemponda akitoa ufafanuzi kwenye semina  ya uhamasishaji iliyoandaliwa na baraza kwa wakuu idara na taasisi mbalimbali za umma na binafsi kuhusu maandalizi ya Mdahalo wa ‘Smart Partnership Dialogue’ unatarajiwa kufanyika hapa nchini hapo Mei 24-28, 2013.
Baraza la Taifa la Biashara  (TNBC) limewata wananchi  kushiriki majadiliano ya biashara ya ushirikiano kwa manufaa ya wote ( Smart Partnership Dialogue) ili kutoa mawazo yatakayo chochea kasi ya maendeleo ya biashara na uchumi hapa nchini.
Kaimu Katibu Mtendaji wa TNBC, Bw.Samson Chemponda alisema hayo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuwa majadiliano hayo  yanayolenga kutoa fursa kwa jamii kukaa pamoja na kuzungumzia maswala mbalimbali ya biashara na maendeleo.
“Majadiliano haya ni muhimu sana na  tunayo makundi nane likiwemo la serikali,wanasiasa, wafanyabiashara, wasomi,wafanyakazi, vijana, wasanii na wakulima ambao wanakaa pamoja na kujadili maswala mbalimbali yanayohusu  biashara na maendeleo,” Alisema Bw. Chemponda.
Bw. Chemponda alikwa akizungumza  katika semina ya uhamasishaji iliyoandaliwa na baraza kwa wakuu idara na taasisi mbalimbali za umma na binafsi, alisema mchakato wa majadiliano ulishazinduliwa na Rais Jakaya Kikwete tangu Mei 29, 2012.
“Madajiliano hayo yatawaleta watu  kutoka  makundi hayo nane ili kujadili kwa kina mbinu zinazoweza kuikwamua nchi kwa kuanisha mambo ya msingi yanayotakiwa kufanyika ili yaweze kuwa msingi wa shughuli za uchumi na maendeleo,”aliongeza.
Alisema baraza kupitia mabaraza ya mikoa na yale ya wilaya ambako madajiliano hayo yatafanyika kuanzia huko hadi ngazi za kitaifa, makundi yote yatapata fursa ya kujadili na kutoa mapendekezo yao.
“Mafanikio ya majadiliano ya kitaifa yatatoa msukumo mkubwa katika utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa miaka mitano,” Bw.Chemponda alisema,na kuongeza kuwa ushiriki wa wananchi kuanzia ngazi za chini ni muhimu sana.
Naye Mwezeshaji  katika semina hiyo,Profesa Lucian Msambichaka alisema lengo la majadiliano hayo ni kuwawezesha wananchi kuzungumza maswala haya maendeleo kwa kina na kuchukua jukumu.
“Nchi yetu ipo chini kiviwanda,sasa ni lazima tuingie katika viwanda vya magari,madawa na vya kusindika mazao ili kuufanya uchumi wetu kuwa imara na kusaidia kutoa ajira,”alisema Profesa Msambichaka.
Alisema majadiliano hayo yatasaidia kupata mawazo na mbinu juu ya kuibua vipaji vya vijana na kuvilinda ili kuleta msukumo wa kuimarisha maswala ya sayansi na teknolojia.
Kauli mbiu ya  majadiliano hayo ni ‘Leveraging/Anchoring Technology for Africa’s Socio-Economic Transfomation: The Smart Partnership Way’ ambayo inalenga kuleta mapinduzi ya uchumi, teknolojia na miundombinu.
Alisema Tanzania imebarikiwa kuwa na kila kitu ikiwemo ardhi nzuri kwa shughuli za  kilimo, maji ya kutosha na raslimali nyinginezo , hivyo kinacho hitajika ni kubadili tabia na kujenga uzalendo katika kulitumikia taifa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Bw.Godfrey Simbeye alisema mdahalo wa ‘Smart Partnership Dialogue’  ambao unafanyika Tanzania  kwa mara ya kwanza unalenga kuboresha mazingira ya biashara.
“Watanzania kwa makundi yao watapata fursa ya kitaifa kuzungumza mafanikio yaliyopatikana na makosa yaliyofanyika ili kujirekebisha na kuchukua jukumu zaidi katika kutekeleza,” alisema.
Alisema serikali itakuwa na wajibu wa kutekeleza yale mapendekezo yote ya makundi hayo na wananchi hao kuchukua jitihada kwa yale yanayowahusu ili kujenga taifa bora kiuchumi.
Semina hiyo iliyoandandaliwa na Baraza ni mwendelezo baada semina za uhamasishaji zenye lengo la kutoa ufahamu kuhusu majadliliano ya kitaifa kabla ya yale ya kimataifa yatakayofanyika hapa nchini kati Mei 24 na 28, 2013. Hivi karibuni baraza liliandaa semina kama hiyo kwa wahariri na waandishi wa habari waandamizi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...