Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda (pichani) leo ametoa Uamuzi juu Tuhuma zinazowakabili Wabunge walio kwenye Kamati ya Nishati na Madini kuhusika na Rushwa katika Utendaji wa kazi zao za Kibunge.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Hivi fedha zilizotumika kwenye mchakato huu zingenunua madawati mangapi ya wanafunzi au kiasi gani cha dawa za hospitali. Muda uliotumika na watendaji kwa hili suala tukiuthaminisha si ungeweza kutumuka kwa mambo mengine ya maana?


    Hivi huko bungeni kuna watu wanafiliria mbali wamapojiingiza kwenye malumbano yasiyo na tija au ni kutopota tu?

    ReplyDelete
  2. Hatukutegemea kitu tofauti na kulindana. Kesi ya nyani umpelekee ngedere unategemea nini?

    ReplyDelete
  3. Hii ngoma angekuwa nayo 6 jamani mbona ingekuwa raha.Prof.Muhongo rudi bwana Geology ukafundishe,sisi tunaokufahamu uchapaji kazi wako tulishajua huko(kwenye siasa) utajishushia hadhi yako.

    David V

    ReplyDelete
  4. sio kila tunavyotegemea lazima iwe hivyo,kuna uwezekano mkubwa huyo katibu mkuu wa wizara ya nishati ni mzushi..!

    ReplyDelete
  5. Kulindana kivipi?kama mtu kaonewa atoke hadharani aseme ushahidi wake.Hii imethibitisha uwongo na kutaka sifa kwa wabunge wetu bila kujali maslahi ya umma

    ReplyDelete
  6. Hanma kitu hapa...ndiyo mana wameanza kujitetea na hizo privilege zao za kibunge....Prof Muhongo ni mtu makini sana kama alivyosema ni ukweli mtupu....mbona wananchi hawakuulizwa? AIBU TUPU. Hata katibu wa Bungu hana credibility aliyo nayo Prof Muhongo...msidanganye wananchi...!

    ReplyDelete
  7. KWA KUWA WATOA MAONI WOTE HUMU NDANI KWENYE HII TOPIC MME KURUPUKA NA KUTOA MAONI BILA KUSOMA TAARIFA YOTE YA SPIKA BASI NATOA ONYO KALI SANA MSIRUDIE SOMA TAARIFA YOTE KWANZA KABLA YA KULIPUKA. OWIII KWELI SAFARI YA TANGANYIKA BADO NI NDEFU SANAAA. YAANI WABUNGE HAWA RUHUSIWI KUONGEA NA MEDIA KITU CHOCHOTE KAMA WAMEAMBIWA BILA KUFANYA UTAFITI WA KINA? BASI KWELI WANA HITAJI KUONGEZEWA MISHAHARA NA MARUPURUPU MAANA SIKU HIZI KUFUATILIA NEWS INABIDI PESA ITUMIKE LOL JUST A SAY....

    ReplyDelete
  8. Matoke ya kila uchunguzi hutegemea ushahidi, sasa wanaoponda sijui walitaka maamuzi ya spika ya base wapi sijui. Maelezo ya spika yameanikwa hadharani, tunataka nini tena , kujiumiza kichwa? ndiyo ile kusema kwamba ukiwa kwenye internet watu hawawezi kujua kama aliendika ni mbwa au panya?

    ReplyDelete
  9. hahah kwa mtizamo wangu binfsi sijaona maamuzi ya spika bali ni ushauri wa spika mfano aliposme ......"Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter M. Muhongo (MB.) anatakiwa awe mwangalifu anapotoa kauli Bungeni, kwa sababu kauli za Mawaziri huchukuliwa kuwa ni kauli za Serikali. Hivyo anapotoa kauli yoyote Bungeni, ahakikishe kuwa ana uhakika wa ukweli wa jambo analolisema" huu ni uamuzi au ushauri kwa mh waziri.

    ReplyDelete
  10. Ushahidi wa rushwa ni kushikwa nayo. Hawa wamekosea kusema tumeombwa wangetakiwa waweke mtego. Wanaweza kuwa kweli waliombwa lakini ushahidi uko wapi. ndio maana ya kuwa na washauri ili pengine iwekwe mikakati kamili kuliko uwe mwenyewe mwenyewe tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...