Mkazi wa Mtaa wa Mbete,Kata ya Isanga Jijini Mbeya Bwana Yussuf Hamad (39), anatuhumiwa kumpa mimba binti yake wa kumzaa (16) jina lake limehifadhiwa. akiingia mahakamani leo mbele yake ni mke wake na mtoto wake aliyezaanae ambao sura zao tumefunika, Kwa picha zaidi wa tukio hilo bofya read more
Bwana Yussuf Hamad anatuhumiwa kuzaa na bintie akitaka kumpokonya kamera mwandishi wa gazeti la majira Rashid Mkwinda ili asimpige picha
Jamaa kuona amezidiwa akaamua kujifunika na shati lake huku akitoa maneno makali kuwa nyie waandishi mmekosa cha kuandika mmeona hii ndiyo habari hakuna habari nyingine? alihoji mtuhumiwa huyo
Huyoooo anatoka nje ya mahakama
Sasa anavaa kofia yake ili watu wasimtambue huku akisema nifuateni niwaonyeshe kazi
Njooni sasa huku kashika jiwe
Kuona anazidi kufuatwa akaamua kuondoka mahali hapo huku akiwa na jiwe lake mkononi
Akina mama wanamsindikiza kwa kumzomea mtuhumiwa huyo
Mkazi wa Mtaa wa Mbete. Kata ya Isanga Jijini Mbeya Bwana Yussuf Hamad (39), anatuhumiwa kumpa mimba binti yake wa kumzaa (15) jina lake limehifadhiwa.
Hayo yamethibitishwa na Mama mzazi wa binti huyo Bi. Regina Simon(35) baada ya kupata taarifa Mei 11 mwaka huu kuwa binti yake ana ujauzito wa miezi minne,na kuamua kutoa taarifa kwa Balozi wa mtaa huo Bwana Steven Ovaova ambaye naye alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kitongoji Bwana Angelo Sanga.
Viongozi hao wa mtaa walimuita mtuhumiwa na ili kupata ukweli wa tukio hilo, lakini mtuhumiwa alikanusha ingawa binti yake alithibitisha kutendewa ukatili huo na kwamba alikuwa akitishiwa kwa mapanga kila alipokuwa akifanya naye tendo la ndoa.
Baada ya uongozi kupata maelezo kutoka kwa binti huyo na mzazi kukataa waliamua kuipeleka kesi hiyo Polisi,ambapo walitoa PF3 iliyomwezesha binti huyo kupelekwa kwa daktari ambaye alithibitisha kuwa binti huyo ana ujauzito.
Binti huyo amejifungua mtoto wa kike ambae sasa ana miezi mitatu mtoto huyo kaletwa leo mahakamani kama ushahidi kesi hiyo imeairishwa mpaka tarehe 12/12 mwaka huu,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Waka test DNA huanda siyo mtoto wake, DNA peke yake ndo itahukumu kesi hii, kwasababu mimi najua akimama hawa tunaishi nao tu wengine, lakini taimingi za kuzaa zote anampelekea mwanaume apendae zaidi. usikatae wako akina mama jeuri namna hiyo, trust me.

    ReplyDelete
  2. Kweli huu ni mwisho wa dunia,ee Mwenyezi Mungu tunusuru.

    ReplyDelete
  3. Wapo Kibao wa baba wanao ffff na binti zao na watoto kuzaliwa au kutozaliwa. Huu uozo upo sana katika jamii zetu. Msimtoe Kafara huyu baba. Wizara husika ifanye utafiti wa kina kuhusi dhambi hii na itoke na mkakati hasa kuimarisha sheria ya masuala ya Kujamiiana ya mwaka 1998

    ReplyDelete
  4. Mangi wa KiboshoDecember 07, 2012

    Mbeya Ina madhehebu mengi mno ya DINI kuliko Mikoa yote TZ., lakini inaongoza kwa mambo yote mabaya kama vile kuchuna ngozi, mauaji ya vikongwe,USHIRIKINA, na mambo yote yanayomchukiza MUNGU! Why nyie Wanyakyusa na Wasafa?

    ReplyDelete
  5. KWELI HATA MIMI NIMESEMA KWA SASA TUNAISHI SIKU ZA MWISHO KABISA. DHAMBI ZA KUNIGILIA WATOTO WA KUZAA MTU MWENYEWE ZIMEKITHIRI NA NINA HAKIKA YESU ANRUDI KUKOMESHA UOZO HUU LAKINI KAZI NI KWETU JE TUMEJITAYARISHA VIPI KUUKABILI USOWAKE YESU?
    MATENDO YA UKATILI KWENYE JAMII YAMEKUWA MENGI KILA KUNAPOKUCHA LAKINI KWA NEEMA YAKE TUTASHINDA
    MUNGU ATAMSHUGHULIKIA HUYU BABA WA BINTI HUYU MDOGO AMBAYE AMEMHARIBIA MAISHA YAKE YA BAADAYE

    ReplyDelete
  6. hapa sasa ndio sehemu sahihi ya kutumia DNA! wampime mtoto ikigundulika ni wa huyo baba ni kifungo cha maisha ndicho kitakachomfaa, jamani wanaume hivi mna nini nyie? mwanao wa kumzaa anakutamanisha nini sasa?

    ReplyDelete
  7. kwa kweli hata mimi imenishangaza na kunisikitisha pia mtoto wako wa kumzaa au ndio mambo ya kishirikina tunayosema mganga kakwambia ili upate mali uende ukatembee na mwanao jamni watanzania tuamke kielimu tusidanganywe ovyo ..
    alafu fikiri kabla ya kufanya kitu ..

    ReplyDelete
  8. Swala hapa sio DNA tu kama baba kamlamba mwanae bila ridhaa yake tena under 18...huyo ni miaka 30 tu!

    ReplyDelete
  9. Kuna mfano hai niujuao mie, dada ana mume wake wa ndoa amezaa mtoto na mwanaume mwingine, na boyfriend wake ana uwezo kwahiyo kaamua mtoto kumpachika ubaba boyfriend kwakua mshiko wa uhakika anao. Kwahiyo mtoto ana baba watatu na wote wanahudumia bila kujua kua wako watatu.

    ReplyDelete
  10. Vutuko anavyofanya atakuwa ni mwenda wazimu tu huyu!

    ReplyDelete
  11. MIMI NADHANI WAZAZI WA NAMNA HII KATIKA JAMII ZETU NI KAMA SUMU,WATU WA NAMNA HII WAWE WANANYONGWA HADHARANI,ILI KUKOMESHA HUU UCHAFU.

    ReplyDelete
  12. Yusuf Hamad,

    Katika umri huo wa miaka 39 ungali bado na Saikolojia ya Punda?

    Hivi kwa kitendo ulichokifanya utakataa usiitwe Punda?

    ReplyDelete
  13. Wewe Mwanaume hapo Jijini Mbeya pana Wasichana wengi tena wa Usiku wasiokuwa na mashariti magumu hela yako tu, tena wazuri sana, kwa nini usiende huko kumalizia shida zako uende kwa mwanao uliyemzaa wewe mwenyewe?

    ReplyDelete
  14. Khaaa!

    Kinyaa sana, ni uchuro mkubwa, hivi baba mzazi unashusha zipu ya suruali yako kumwelekezea mwanao uliyemzaa mwenyewe?

    Au ndio mashariti ya Waganga umepewa ili kuusaka Utajiri?

    Ndio maana maafa ni mengi sana siku hizi!

    ReplyDelete
  15. Watu kama hawa Yusuf Hamad wa Mbeya na mambo ameyafanya ndio wanasababisha mvua zinakuwa adimu hazinyeshi na hata kama zikinyesha zinaleta mafuriko!

    ReplyDelete
  16. Moyo alionao baba huyu ni mgumu sana!

    Kwa kawaida watoto wako wa kike wanakuwa ni sawa na mama yako wewe Yusuf Hamad na wa kiume ni sawa na baba yako wewe Yusuf Hamad.

    Sasa kwa kitendo chako kwa Binti yako huna tofauti na kumfanyia tendo hilo mama yako mzazi wewe Yusuf Hamad!

    ReplyDelete
  17. Huyu jamaa hakuna haja ya kupimwa DNA ni wazi tendo amelifanya kutokana na majibu anayoyatoa kuwafokea Waandishi wasichukue Taarifa za tukio hili hapo Mahakamani.

    Ohhh anajifanya anafoka wakati picha ya kwanza hapo juu Waandishi wamempiga akiwa hajijui, eti chini anajifunika na shati kake kuficha aibu!

    Je, umekuwa ndege Mbuni anayeficha kichwa chake kwenye rundo la mchanga huku mwili mzima ukiwa nje?

    Ahhh jamaa huyu ana moyo mgumu sana !

    ReplyDelete
  18. Mwisho wa ubaya ni aibu!

    ReplyDelete
  19. Mume bwege ameimbwa katika wimbo, sasa leo huko Mbeya amepatikana huyo baba bwege!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...