DSM City Press Club imepata taarifa  za kushtusha kufuatia ya kupigwa risasi  na kujeruhiwa begani kwa mwandishi wa Tanzania Daima Bwana Shabani Matutu (30) ambaye pia ni mwanachama wa Dar City Press Club
(DCPC). 

Sambamba na taarifa hizo imeelezwa kuwa mwandishi huyo amelazwa katika Taasisi ya mifupa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MOI). Chanzo hasa cha kupigwa risasi kwa mwandishi huyo bado hakijaeleweka kwa DCPC, uongozi wa DCPC unafuatilia.

Tutakapojiridhisha na taarifa zilizotolewa pamoja na zile tutakazozipata tutawataarifu rasmi. Kwa sababu hizo tunaomba waandishi wote, ndugu, jamaa, marafiki, wapenda haki na amani , wanaharakati washirika na wadau wote wa vyombo vya habari kuwa watulivu tukimjulia hali kwa misaada ya hali na mali mwandishi mwenzetu Shabban Matutu ili apone majeraha.

Wenu katika ujenzi wa Taifa,



Joseph Kayinga
Katibu Mkuu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...