Bendi maarufu ya mziki wa dansi barani Ulaya "Ngoma Africa" aka FFU Ughaibuni, Inawatakia kila la heri na fanaka waTanzania wote kwa kuadhimisha miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania (bara).
Uongozi wa bendi hiyo unaiombea kila la heri, Serikali ya Tanzania,Wananchi na Taifa la Tanzania.
Katika kusherekea miaka 51 ya Uhuru,Ngoma Africa band inawaombea wadau na wananchi wote popote walipo,kutumia wakati huu kujikomboa kimawazo,na kuhakikisha kuwa tunajenga na kudumisha umoja,mshikamano na upendo wa kitaifa,hili kuleta maana kamili ya "Uhuru" wa maisha ya Mtanzania.
Katika Kusherekea miaka 51 ya Uhuru, watanzania tunapaswa zaidi kujenga
na kuziba nyufa zinazo bobomoa au kujaribu kubomomoa msingi wetu imara wa umoja,pendo na mshikamano wa kitaifa.
Mungu Ibaraki Tanzania !Mungu wabariki Watanzania !
Mungi Ibariki Serikali ya Tanzania !
Tafadhali pata burudani kamili at www.ngoma-africa.com
Ahsanteni sana wana wa Makunjas kwa salamu nzuri kabisa na za Kizalendo za miaka 51 ya Uhuru!
ReplyDeleteAsanteni sana maafande wa FFU,kwa ujumbe wenu mzuri kwa taifa na watanzania
ReplyDeleteKamanda Ras makunja mie nipo nation studium nangojea kuona ligwaride lenu
ReplyDeletemkiwa na magitaa mikononi