Huduma ya M-Pesa ilipata hitilafu jana…Wahandisi wa mtandao Tanzania wakishirikiaana na wadau wa nchini Uingereza walifanya kazi usiku na mchana ili kutatua tatizo na hatimaye kuwezesha huduma kufanya kazi mida ya jioni.

Mkurugenzi  wa kitengo cha M-Pesa, Jacques Voogt  amesema  wateja walikua wakipiga  *150*00#   wanapata ujumbe mfupi SMS usemao “Ndugu mteja, huduma ya M-Pesa haipatikani kwa sasa, tafadhali jaribu tena”
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kwa wateja wetu, mawakala wa M-pesa na wadau wetu wote kwa ujumla.

M-Pesa ni huduma pendelevu ya malipo kwa wateja zaidi ya milioni 4.5 na ina wadau wa biashara zaidi ya 200 wanaotumia huduma hii kukusanya na kusambaza pesa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...