Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Magesa Mulongo akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kisima kirefu cha maji kilichochimbwa na Kanisa la International Evangelism(IEC) kwenye hospitali ya wilaya ya Meru mkoa wa Arusha.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Mhe. Joshua Nassari akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuzindua kisima kirefu cha maji kwenye hospitali ya wilaya ya Meru,kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo na Askofu Mkuu wa Kanisa la International Evangelism,Dk Eliud Issangya.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Meru,Aziz Msuya akizungumza wakati wa uzinduzi wa kisima kiirefu cha maji katika hospitali hiyo kilichochimbwa kwa gharama ya shilingi milioni 19 kwa ufadhili wa Kanisa la International Evangelism(IEC)ili kuondoa kero ya maji iliyokuwa ikiwasumbua kwa muda mrefu.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Magesa Mulongo akifungulia maji kwenye ndoo wakati wa hafla ya uzinduzi wa kisima kirefu cha maji kilichochimbwa na Kanisa la International Evangelism(IEC) kwenye hospitali ya wilaya ya Meru mkoa wa Arusha,anayeshuhudia ni Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassari.
Mkuu wa Moa wa Arusha, Mhe. Magesa Mulongo(wa pili kushoto)akifurahia jambo pamoja na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Mhe. Joshua Nassari mara baada sherehe za uzinduzi wa kisima cha maji katika Hospitali ya wilaya ya Meru wengine kutoka kushoto ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Meru,Aziz Msuya,Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM,Juliu Mungure na mkuu wa wilaya ya Arumeru,Nyirembe Munasa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...