Kontena  lililosheheni kondomu za kiume kutoka nchini India limekamatwa na kuzuiliwa katika Bandari ya Dar es Salaam, baada ya kubainika kuwa hazifai kwa matumizi ya binadamu.
Maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wamelazimika kufanya msako mkali kwenye baadhi ya maduka ya dawa jijini Dar es Salaam baada ya kubainika kwamba tayari kondomu hizo zipo sokoni.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Leandri Kinabo alizitaja kondomu hizo kuwa ni aina ya Melt Me zenye thamani ya Sh222.1   milioni zilizokamatwa tangu Oktoba 23 mwaka huu na kuzuiliwa bandarini hapo kwa taratibu zaidi za kisheria.
“Jambo lililotushtua ni kwamba zimebainika kwamba zipo madukani, tukajaribu kufuatilia tena bandarini tukifikiri kuwa huenda zimetolewa kinyemela licha ya kuzuiliwa ili ziteketezwe au zirejeshwe nchini India kwa gharama zao wahusika.
Tulipokwenda bandarini tukabaini kwamba bado zipo katika hali ile ile, kumbe  zimeingizwa nchini kwa njia ya panya, kwa kweli ni mbovu na ndiyo maana tumelazimika kuwajulisha wanahabari ili muwape taarifa wananchi wawe makini,” alisema Kinabo.
Alifafanua zaidi kwamba kondomu hizo ni mbovu kwani zimebainika kuwa na vitundu, pia zinapasuka haraka, hazina kabisa viwango vya ubora wa bidhaa unaotakiwa na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO).
Kinabo alisema kuwa TBS bado wanaendelea kufanya mawasiliano na kampuni iliyotengeneza kondomu hizo, lakini kwenye kasha  lake inaonyesha kuwa inaingizwa nchini na kampuni ya Fair Deal Exim ya Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Jamanihii nchi tunaelekea wapi sasa.Mimi nashauri katika kipindi hiki cha mpito huku tukisubiri vyombo husika viteketeze ama kurudisha shehena hiyo India ni vema "TUNGEACHA KIDOGO MAMBO YA NGONO" mpaka hapo kondom fake zilizopo madukani zimeondolewa na kuteketezwa kabisa.

    ReplyDelete
  2. jamani hapo bandari ya Dar es salaam tusipokua makini watanzania tutakufa woote..haiwezekani mtu mmoja au kikundi cha watu wachache kwa ajili ya ufisadi wao waangamize taifa..

    kwa nini watu hao wasinyongwe tu??..tunamshukuru Mwakyembe kwa kuisafisha hio bandari..timua watu wote wasio waadilifu...kuna watu wapo mtaani wanahitaji kazi..watu washazoea hizo kazi na wanafanya wanavyotaka,,,timua wote wachafu,,nyonga wote hao,,

    ReplyDelete
  3. Hizi zilikuwa tayari kwa ajili ya kuuwa watu. Duh, Ubinafsi ni noma kweli ,watu wala hawajali kabisa. Wanasahau wana ndugu zao, au watoto wao watazitumia pia . Tanzania imefikia pabaya sasa.

    ReplyDelete
  4. habari hii bado haijakamilika, ilipasa mwandishi atuambie majibu kutoka fair deak exim kuhusu hizo condom zao feki, alafu tulitaka mwandishi atoe majibu baada ya kuwaoji mamlaka husika ni hatua gani za kisheria zitafuata kama zipo na kama hazipo nini wanatarijia kufanya! Zaidi ya hapo atakua kama ma-repoter wengine tu!

    ReplyDelete
  5. kwani lazma kufanya ngono zembe?dawa ni kuowa/kuolewa.wacha wazinifu waendelee kuteketea

    ReplyDelete
  6. Ahhh,

    Kwa nini tusirudi kwenye swala?

    Ngono sasa basi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...