Hii ni Mashine ya Unga ilIyotengenezwa na Wajasiriamali wadogo wadogo katika Mkoa wa Mwanza, nayo vilevile inapatikana kwenye Maonesho hayo na Picha namba 1010240 mashine husika inafanyiwa majaribio.

Maonesho ya Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) yanayo fanyika jiji Mwanza katika Viwanja vya Nyamagana, yameonekana kuwa kivutia kikubwa kwa wakaazi wa Jiji hilo, Mwandishi wa Blog hii alivyofika alishuhudia bidhaa mbalimbali zilizo tengenezwa na Wazalendo wa nchi hii zikwa zimepedeza, nakufanya kununuliwa na wadau Mbalimbali waliofika kujionea Maonesho hayo.

Katika siku za hivi karibuni Mkoa wa Mwanza umeendelea kuwa kivuti kikubwa hasa katika suala la Uwekezaji kwani Mkoa huo Unatajwa kukuwa kwa kasi kubwa Miongoni mwa Miji iliyoko kusini Mwa Jangwa la Sahara.

Kwa upande mwingine Mkuu wa Mkoa huo Evarist Ndikilo, Mapema wiki hii akifungua Mkutano wa Kutathmini Malengo ya Millenia kwenye Hotel ya Gold Crest alisema Amani ni suala muhimu sana katika kujiletea Maendeleo, hivyo akawaasa wana Mwanza na watanzania kwa ujumla kuhakikisha wanailinda hali ya utulivu iliyopo, kwana itasaidia wana Mwanza kujiletea Mandeleo kwakufanya shughuli zao bila yakuwa na wasiwasi.

Baadhi ya wajasiriamali wakiwa katika Viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza Wakionesha Bidhaa zao.
Ni sehemu tu ya Wajasiriamali wadogo wadogo, wakiwa wanaonesha sehemu ya Bidhaa wanazo zalisha katika Viwanja vya Nyamagana.
Dagaa wa Ziwa Victoria wamekuwa kivutio kikubwa kutokana na Umahiri wa Wafanyabiashara hawa wadogo walivoweza kuwafunga kwenye karatasi nzuri za nailoni nakupewa Garantiii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...