Mwezeshaji wa mafunzo ya siku tatu kwa waandishi wa Habari juu ya Wajibu wa Vyombo vya Habari katika utekelezaji wa Soko la Pamoja la Jumuia ya Afrika ya Mashariki (EAC), Balozi Jeremy Ndayiziga, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo hayo yaliyoliyoanza leo Jijini Dar es Salaam na kushirikisha waandishi kutoka nchi Wanachama wa EAC. Kulia ni Mtaalam wa Masuala ya Habari kutoka EAC, Sukhdev Chhatbar, ambaye pia ni mratibu wa mafunzo hayo. Balozi Ndayiziga ni Mtaalam katika Masuala ya Mtengamano wa EAC.

Mtaalam wa Masuala ya Habari kutoka EAC, Sukhdev Chhatbar, ambaye pia ni mratibu wa mafunzo hayo akijadili jambo na Mwanahabari Mkongwe na Mchambuzi wa Masuala ya Siasa za Afrika, Jenerali Ulimwengu. Ulimwengu pia ni Mwezeshaji katika Mafunzo hayo.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...