Rais wa COP18 na wenyeviti wa kamati mbalimbali katika mkutano wa mawasilisho ya nchi katika siku ya mwisho ya mkutano wa nchi wanachama duniani wa mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi uliokuwa ukifanyika mjini Doha na majadiliano mengine yakiendelea katika kumbi tofauti.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Zanziar,Dkt. Shajak Omary (wa pili kulia) na (kushoto) Naibu katibu Mkuu wizara ya kilimo Zanziabar,Dkt. Assad wakifuatilia mawasilisho yaliyokuwa yakiendelea kwenye mkutano huo.
Katibu Mtendani wa Tume ya Mipango Zanzibar,Bi Amina Shaaban na Mh. Bernadeta Mushashu (kulia) Mbunge wa Bunge la Afrika, ambae pia ni Mbunge Viti Vaalum CCM Kagera na ni mjumbe wa kamati ya maliasili na mazingira wakifuatilia kwa makini mawasilisho hayo.
Wenye mashati meupe, mbele Bw. Owden Kasongwa mkurugenzi msaidizi idara ya mipango Ofisi ya Makamu wa Rais, nyuma mkurugunzi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt Julius Ningu wakifuatilia mawasilisho.(Picha zote na Evelyn Mkokoi)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...