Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Zahor Kassim Mohamed EL-KHAROUSY kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi katika Bahari Kuu.

Taarifa iliyotolewa na kutiwa saini leo, Ijumaa, Desemba 7, 2012 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa uteuzi wa Bwana El Kharousy ulianza Novemba 28, mwaka huu, 2012.

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Kharousy alikuwa Naibu  Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
7 Desemba, 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...