Mbaraka Mwinshehe na mkewe, Amney Shadad, siku ya ndoa yao tarehe 17/3/1972 mjini Morogoro.Unajua nani alitumwa kama Mshenga?

Na Jeff Msangi, 
Bongo Celebrity
Juzi rafiki yangu mmoja alinipigia simu na kuniuliza “Jeff, unajua jinsi ya kuandika Barua ya Posa?”. Lilikuwa swali la ghafla na hivyo ili kupata muda wa kutafakari kidogo, nami nikarudishia kwa swali “Kwanini, wewe barua ya posa ya nini?”.Akaniambia “swahiba wangu fulani anataka kuoa na hivyo tunahitaji kupeleka barua ya posa kwa wazazi wake”. Nikawa mpole. Ukweli ni kwamba sijawahi kuandika Barua ya Posa. 
Nimeshawahi kuandika barua za kila aina lakini sio ya Posa. Lakini kwa kuelewa kwamba rafiki yangu ameniuliza kwa sababu anajua mimi ni mwandishi na napenda changamoto za uandishi, nikamwambia basi atulie tu na kabla jua halijazama, atapata Barua ya Posa ambayo yeye na mwenzie wataipeleka na kisha kukaa wakisubiri majibu kwa hamu ya ndio au hapana. Ukiaminiwa na jambo fulani kuna sababu na hivyo kama linawezekana,basi lifanye.Urafiki ni kitu muhimu na adimu.
Nilichokifanya baada ya kukata simu ya rafiki yangu ni kuwasiliana na baadhi ya marafiki zangu wengine ambao najua kwa kiasi fulani bado wangali wakizingatia mila na desturi ingawa ukweli ni kwamba katika zama hizi za kukutana na kuachania katika Facebook kabla hata ya kuonana ana kwa ana, inakuwa ngumu kidogo kudumisha mila na desturi. Ni dunia ambayo endapo mababu zetu waliotangulia mbele za haki wanatuona tukihangaika nayo, basi wanajionea maajabu tu. Ni tofauti sana na ile waliyoishi wao. 
Kusoma makala yote na kusikiliza kibao cha 'Mshenga namba moja' cha Mbaraka Mwinshehe Mwaruka BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kweli ndugu, utandawazi umetumeza mno. Ingefaa mtaala wa shule somo la maarifa iwemo mada ya "NAMNA YA KUANDIKA BARUA YA POSA" AU "KUDUMISHA MILA"

    ReplyDelete
  2. Aise asante mdau Jeff.Sasa hivi ni utandawazi bwana barua za posa za nini,ni fb tu kwa kwenda mbele!!Ila siyo siri hawa mababu zetu waliishi maisha `simple` sana na yenye raha.Picha ya harusi yenyewe iko simple na nzuri sana.Ilikuwa burudani kweli.

    David V

    ReplyDelete
  3. Mdau umekuja na mada muhimu sana, kwa kipindi chetu cha Kizazi hiki jukumu la barua limebakia kwa Viongozi wa Dini na Wazee majumbani.

    Waoaji Masela na Mabitoz wa siku hizi wengi wao hata ujuzi wa kujieleza ukweni hawana, wanategemea kushindikizwa siku ya Tukio husika na ukiwakuta pale ,ohhhh wanakuwa wapoleeee, ujanja kwisha!

    Unajiuluza hivi huyu ndiyo yule yule mbishi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...