Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza kufungua kikao cha dharura cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kwa ajili ya kupokea na kujadiili taarifa ya uchunguzi wa mgogoro kati ya muwekezaji katika shamba la malonje ambaye ni Ephata Ministry na wanakijiji wanaolizunguka shamba hilo wa vijiji vya Malonje, Skaungu naMawenzusi leo katika ukumbi wa RDC unaomilikiwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo. Taarifa hiyo iliandaliwa na kamati aliyoiunda Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kuchunguza juu ya sakata hilo. Kulia na Katabu Tawala wa Mkoa huo Alhaj Salum Mohammed Chima.

Baadhi ya wajumbe halali wa kikao hicho. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini Ndugu Ali Kesi, watatu kulia Mbunge wa Jimbo la Kwela Ndugu Iganas Malocha, Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Ndugu William Shimwela na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Godfrey Sichona.
Wajumbe wa kikao hicho vyombo vya ulinzi na usalama.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akisoma taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa shamba la Malonje la muwekezaji Ephata Ministry na wananchi wa vijiji jirani na shamba hilo leo katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo(RDC), taarifa hiyo iliwasilishwa na kupokelewa na wajumbe wa kikao hicho ambacho kwa ujumla waliipongeza kamati iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa huo kuchunguza sakata hilo linaloibua sura mpya katika vipindi tofauti.
Mshauri wa Kitengo cha Serikali za Mitaa katika Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa Ndugu Francis Ikayo akichangia katika kikao hicho.
Mratibu wa mradi wa afya ya mama na mwana kutoka shirika lisilo la kiserikali la kimataifa la Africare Ndugu Gasper Materu akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi unadhaminiwa na shirika hilo Mkoani Rukwa. Katika taarifa yake hiyo alisema kuwa jumla ya wahudumu wa afya 2880 katika ngazi ya jamii wameshapatiwa elimu juu ya mpango wa uzazi salama kupunguza vifo vya mama na watoto Mkoani Rukwa. Aliongeza kwa kusema kuwa washiriki wote hao wamewezeshwa baiskeli ili kuweza kuzungukia kaya mbalimbali katika maeneo yao ili kuwafikishia wananchi wengi zaidi elimu hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...