Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wahindu Tanzania Bw. Ramesha Patel akimpokea na kumtambulisha mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa wakati alipowasili kwenye msikiti mkuu wa Dhehebu hilo ulioko jijini Dar es Salaam kwa shughuli maalum ya kuliombea taifa Amani.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akiingia katika msikiti wa dhehebu la Wahindu kuhudhuria ibada maalum ya kuliombea taifa Amani.
Waendesha Ibada maalum kutoka India katika moja ya hatua za ibada hiyo wakimpa baraka za namna ya pekee Mstahiki Meya Jerry Silaa.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akishiriki kuomba dua na waumini wa dhehebu hilo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza na wanajumuiya ya Hindu ambapo amewashukuru kwa kumkaribisha kuungana nao katika Ibada hiyo maalum na kuwataka kuendelea kuwa na mshikamano na jamii nyingine pamoja na Serikali.
Mstahiki Meya ametumia fursa hiyo kuwataka wanajamii hiyo pale wanapokwama au kukwazwa kibiashara katika manispaa ya Ilala kwa jambo wanaloona linaweza kutatuliwa wasisite kuwaona viongozi wao na kuwaambia viongozi wao wasisite kumuona yeye moja kwa moja ili watafute ufumbuzi kwa manufaa ya Manispaa na jiji kwa ujumla. Kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Ramesh Patel.
sio msikiti ni hekalu.
ReplyDeleteToka lini msikiti ukawa mahala pasalaa ya dini ya HINDU?Tumieni majina yaliokuwa sawa.
ReplyDeletejamaa na waheshimu sana, hakuna mzungu au muarabu aliyewateteresha katika imani zao. Sisi waafrika tumebaki kubeza jadi zetu na kuona za wenzetu ndio bora kabisa.
ReplyDeleteNa wewe kajiunge basi na hao waisotetereshwa kwani umeambiwa lazima ufate hao waarabu au wazungu
ReplyDelete