Ikiwa ni takribani miezi minne tangu tawi la CHADEMA UK lifunguliwe rasmi na Mr Godbless Lema, kumekuwepo na maendeleo makubwa ya ujenzi wa tawi hili lakini vile vile kumekuwepo na changa moto mbali mbali kutokana na uelewa wa watu ktk dhana nzima ya M4C. M4C ikiwa na maana ya Movement for Change, ni sharti mtu yeyote anayeingia ktk movement hii kwenye ngazi ya uongozi aelewe haya machache ya msingi:
1)   Kwanza aone matatizo yanayomgusa yeye na jamii yake
2)   Ajue na kutambua fika chimbuko la matatizo haya
3)   Awe tayari kuwa kiini cha mabadiliko ya kweli anayoyataka kwa jamii
4)   Aweze kutoa ufumbuzi kwa kukemea maovu, kuelimisha na hata yeye binafsi kuelimika
5)   Ili afanikiwe ktk kipengele cha (4) ni sharti ajitambue yeye binafsi ya kwamba ni:
i)            Lazima awe safi na mwenye sifa za kukemea waovu
ii)           Aweke maslahi ya jamii mbele na si yake binafsi
iii)         Awe na sifa za uongozi zinazotakiwa, nidhamu ikiwa nambari moja ktk orodha.
iv)         Awe na msimamo wa kiitikadi
Kwa hiyo, uongozi wa CHADEMA UK kwa baraka za watetezi wa haki ya kweli (CHADEMA TZ) unawatangazia umma watanzania kokote mlipo kwamba kuanzia leotarehe 12/12/12, Mr Christopher Lukosi (pichani juu) amevuliwa rasmi uongozi na amesitishwa uanachama kutokana na kutokidhi mengi ya yaliyotajwa hapo juu.
Uongozi wa CHADEMA UK unamshukuru sana kwa mchango na ushirikiano wake mkubwa kwa kipindi ambacho matundu ya chujio yalikuwa makubwa. Tutaendelea kumkumbuka na hata kutumia misemo yake yenye maana nzito kwa jamii ya kitanzania, kama vile: -
i)            Sisi sote ni ndugu, tatizo ni CCM
ii)           Kila kwenye msafara wa mamba na kenge wamo
Uongozi unamwakikishia Mr Christopher Lukosi kwamba mamba wote wa CHADEMA UK kwa kushirikiana na wote wenye kuelewa mageuzi ya kweli, tutaliondoa tatizo ifikapo 2015. Tunamtakia kila la kheli katika maisha na ni imani yetu tutaendelea kuwa ndugu yake baada ya tatizo kutatuliwa !!!!.
“We fail in most of our endeavours because we too often underestimate People’s Power” [M4C UK, 2012]

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa



  1. Chadema Chademaaa hahaaaa this is soo funny wakati mnachagua mlikua wapi??
    useless kabisaa

    ReplyDelete
  2. Chris naona wamekutenda wanaCHADEMA, rudi CCM maana kwa CV yako utapokelewa tu pasipo wasi achana na hao watu makini sana.

    ReplyDelete
  3. Sasa huyo kenge atakuwa nani?sidhani kama hata kijiji mnafaa kuongoza ni mapema sana.Msiwe na tabia ya kiboko ni mnyama wa ajabu sana.Mtafukunzana wote hapa uk.Muda mfupi tu huu, kenge wa kwanza kafukuzwa,Je? mkipewa nchi kama mnavyoota ndoto zenu, mtafukunza kenge wangapi?

    ReplyDelete
  4. kweli chadema kwishenea bongo vurugu UK vurugu ntie vipi sasa mtatuendeshea nchi kivipi, vilaza hebu mkalime kama siasa zimewashinda.

    ReplyDelete
  5. Chris ni mfanyabiashara hivyo usipoteze wakati na vyama vya kimasikini njoo hapa Beds ujiunge na Tory upate kutajirika. Sasa Tory wanatafuta Blacks waliofanikiwa kibiashara ili washinde chaguzi zijazo.

    ReplyDelete
  6. Safi sana...hamna kitu huyu jamaa...anafikiri m4c ni kama serengeti freight forwarders...afadhali wamemdondosha

    ReplyDelete
  7. Hahaha..ni lini Mwenyekiti wa Republican-Tanzania atavuliwa madaraka..fanyeni kilichowapeleka nje achaneni na siasa. nyie mliofika nje tulitegemea ndo mngekuwa wakwanza kuelimisha watanzania kuwa uchama hauna deal, deal ni uzalendo...lakini kila mahali ccm, chadema x1000..udinix10000..fanyeni kazi kwa bidii acheni kutafuta umaarufu ambao hauna deal na mtakuja ujutia baadae..Mi MTANZANIA BWANA..SIO CHADEMA WALA CCM..TUNASUBIRIA ISSUE YA MGOMBEA BINAFSI KWA MAPENZI YA MOLA

    ReplyDelete
  8. Kumbe nae mmoja wa MaKenge huyo Eeeh!Anapaswa Kuwajibishwa,safi sana Jeez hapa Washimgton DC USA.

    ReplyDelete
  9. haya sasa chadema wameshaanza kujistukia mtahisi mara zitto nae katumwa ni cm,mara slaaa,mbowe sasa muda si mrefu mtaanza kutafunana wenyewe kwa wenyewe, dhambi ya ubaguzi!!!

    ReplyDelete
  10. hakuna msafi asilimia 100 hapo

    ReplyDelete
  11. Ukiingia CHADEMA uwe makini kwani hiki chama watu wake ni MAKINI mno! hawana ubabaishaji kama CCM.

    ReplyDelete
  12. Haiwezekani kumfukuza kama kuku mdingi namna hiyo, mtu makini najua hata kijiji chake pale rombo.Asikubali mpaka kielewee? kieleweke kweli.

    ReplyDelete

  13. Japan pia kunafuka moshi..
    Watanzania wa sasa siyo kichwa cha mwendawazimu tena kama zamani

    ReplyDelete
  14. Chadema msitake kujifanya mpo safi wengine!

    Sasa kama suala ni M4C mngeanzia kwenye Ngazi ya Taifa badala ya kwenye Tawi tena le nje ya nchi!

    Kama mngeanzia ngazi ya Taifa nadhani Slaa na Mbowe mngewanyang'anya Madarala na kuwavua uanachama ni vile wamesimama kugombea Uraisi mara kadhaa kila mmoja na wakashindwa vibaya kabisa!

    Kama suala ni vigezo ni kujituma na kufikia malengo Mbowe na Slaa wangefaa kuwajibishwa badala ya Christopher Lukosi wa Tawi UK.

    Au kwa vile sio Mchagga???

    ReplyDelete
  15. Chadema waongo na wanafiki, toeni sababu ya ukweli hapo mmebabaisha tu, mara ooooh M4C mara. ohhhh kwenye Kenge Mamba wapo !

    Ohhh,


    Ohhh,

    ReplyDelete
  16. Mwenye kutaka Uongozi CHADEMA,,,Movement for change kwenye ngazi ya Uongozi aelewe haya machache ya msingi:

    1.Kwanza aone matatizo yanayomgusa yeye na jamii yake.

    2.Ajue na kutambua fika chimbukomla matatizo haya.

    3.Awe tayari kuwa kiini cha ukweli cha mabadiliko anayoyataka katika jamii.

    4.Aweze kutoa ufumbuzi kwa kukemea maovu, kuelimisha na hata yeye mwenyewe kuelimika.

    5.Ili afanikiwe ktk kipengele cha (4) ni shariti ajitambue kwamba yeye binafsi ni:
    i-lazima awe safi na sifa za kukemea maovu,
    ii-aweke maslahi ya jamii mbele na si yake binafsi,
    iii-awe na sifa za uongozi zinazotakiwa, nidhamu ikiwa ni namba moja ktk orodha.
    iv-awe na msimamo wa itikadi

    ___________________________________
    HAPO KATIKA No.5 CHADEMA MMEFUNIKA VIPENGELE HIVI AMBAVYO KWENYE MAKABRASHA YA SIRI YA CHAMA CHENU VIPO:

    v-ni lazima awe MCHAGGA ama anatokea KANDA UA KASKAZINI

    Vi-ni lazima atetee maslahi ya Wachagga na KANDA YA KASKAZINI.

    vii-ni lazima ahakikishe nchi inaangukia mikononi mwa watu wa Kanda ya Kaskazini Uchaguzi ujao 2015 bila kujali sifa za Mgombea huyo.

    SASA VIPENGELE HIVYO No.5 kuanzia v,vi, na vii (ambavyo vipo kibindoni kwenye makabrasha ya siri ya CHADEMA) huyo CHRISTOPHER LUKOSI NDIVYO HAKUTIMIZA, HIVYO NDIO HOJA ZILIZOPELEKEA KUVULIWA MADARAKA PIA NA UANACHAMA, SIO OHHH NDANI YA MAAMBA KENGE WAPO ,OHHH ,OHHH, OHHH,!

    NINI SASA?

    ReplyDelete
  17. Asingekuwa Christopher Lukosi akawa CHRISTOPHER MUSHI ,angalau angebaki ktk chama ingawa akiwa hana hata Madaraka!

    ReplyDelete
  18. Mnhhhh!

    Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015 Chadema mmeanza kuweweseka!

    Kweli Uraisi wa nchi mlioukamia mtaupata huku mkionyesha Siasa za ki-Ubaguzi, na ki-Kanda?

    ReplyDelete
  19. Sishangai jamaa ana kauli chafu balaa. Ana dharau kwa kila mtanzania anayebeba box.

    ReplyDelete
  20. Huyu jamaa ni sifuri (zeroooo asilimia mia moja);
    Nilisikitika na kulia kwa uchungu niliposikia ni mwenyekiti wa Chadema UK;Chadema mlikosa watu kabisa??Mbona watu wa maana wanaofaa kuongoza ni wengi tu UK?Mkachukua hiki kiazi!,ni kilaza na hajui kabisa kuongea (interact) na watu.Hongereni kwa kuvua gwanda la kikenge Lukosi.PEOPLES POWERS.

    ReplyDelete
  21. CHRIS LUKOSI HUYU NI MUHEHE,MTOTO WA MZEE LUKOSI ALIYEKUWA OFISA WA CUSTOMS MWANZA?NA NDIYE WA SERENGETI FREIGHT FORWADERS?

    ReplyDelete
  22. Jamaa shushushu, kazidiwa speed na wenzie wamemwingiza bafuni. Kaachwa mdomo wazi maana kwa akili yake ndogo (na arrogance) alifikiri ni mjanja sana. Huwezi kuwafanya wenzio wooote wajinga - wamekustukia, unaanza ooooh chris ana hela, ooooh, kafanikiwa kibiashara. Hapa suala ni hivi: LUKOSI NI SHUSHUSHU, AMEJAA HASIRA, KARAHA, USEMAJI HOVYO, AKILI NDOGO.
    Anaweza kufanikiwa kwenye kupeleka containers dar, lakini sio suala la kutumikia watu.

    ReplyDelete
  23. Kwa Itikadi ya Chadema ya Mapanga mkononi?

    Ni bahati nzuri sana ya kuwa Tanzania na UK ni nchi ambazo kuna Rule of LAW na Social Justice!

    Isingekuwa hivyo, yule Kada wa Chadema aliyempigia Saluti Raisi JK kwenye ufunguzi wa Hospitali juzi kule Sinza Dar, na huyu Christopher Lukosi wa kwenye Tawi Uingereza wangekuwa ,KWA MAKOSA WALIYO YAFANYA (Sinza-Kumpigia Saluti Raisi wa CCM, na UK-Kwa sababu wanazojua Chdm juu ya Christopher Lukosi),,,TUNGEKUTA, KAMA SI KIUNGO NYETI, MASIKIO YAO YAMEKATWA KAWOSHI KWA MAPANGA!

    ReplyDelete
  24. chadumaaa eti ndio wapewe nchi ha haaa, bora shetani anayekujua kuliko malaika asiekujua!! Nzala tupu hao chadumaa

    ReplyDelete
  25. Chris endelea na kazi ya kusafirisha vitu vikakuze uchumi TZ. Hiyo kazi ya heshima kuliko kuwa kiongozi wa vyama vya kisiasa. Hongera kwa kupata uhuru wa maisha yako. Waachie wanaoweza biashara ya kudanganya wananchi (CCM na CHADEMA wote sawa tu!)

    ReplyDelete
  26. Misupu umeanza unabania maoni, acha hizo, hamna mtu aliyetukana hapa.

    ReplyDelete
  27. mnamfukuza kwa makosa yapi? mbona mna generalize? mtaje makosa yake otherwise mtaonekana mna sababu zenu za kinafiki

    ReplyDelete
  28. chama cha mtei nyie si mnatabia ya kuwekana mtoto wa mjomba sasa weken ndugu yenu uk maana ndio tabia yenu hii mijitu ya kichanga sijui itaelimika lini na huo ubaguzi wao, chama kilikua kimekufa long time,kama mzee mtei wezi wakubwa nyie nendeni kwa sabodo awaonge hela kama kawaida yenu

    ReplyDelete
  29. CCM OYEE CHADEMA HAWAELEWEKI WOTE WAKO KWA AJILI YAKUTAKA NYAZIFA TU HAMNA LOLOTE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...