Wakati kumbi za madisko zikiwaka moto kwa ngoma kali enzi hizo,  kwenye majumba ya sinema jijini Dar na kwingineko mambo ya sinema za kihindi yalikuwa juu miaka ya 80 katika majumba ya Odeon, Cameo, New Chox, Empress, Empire, Avalon hata pale Msasani Drive-in (mnaangalia sinema nje bila kusikia sauti, ila kuna mabingwa walikuwa wanakuhadithieni muvi yote kwa kimatumbi). Steringi aliyetamba sana mmoja wao ni Amitabh Bachchan ambaye mbali na kurusha mangumi pia alikuwa anatambna sana kwenye kuimba, mfano ikiwa ngoma hii ya 'Rote Rote Hasna Seekho - Andhaa Kanoon' Wenye data na kuweza kutafsiri msaada tutani pliiizzzz...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. hee heeee heeee Rote Rote Hasna Seekho....mmmh nilikuwa Form I bwenini mahali fulani..ndiyo kwanza nimetoka kijijini nashangaa Video,mara ya kwanza kuiona....Asante Ankal kwa kumbukumbu.Lakini hadi sasa hivi hizi Filamu za kutoka India bado 'zinatesa' sehemu fulani fulani za nchi.

    David V

    ReplyDelete
  2. Hapo waharibifu badala ya kusema 'Rote rote' wao wanasema,,, LOOTE LOOTE !

    ReplyDelete
  3. Du asante sana... umenikumbusha mbali sana... Mjomba wangu alikuwa akuimba huu wimbo sana... jamani nangojea tafsiri yake....

    ReplyDelete
  4. ***** Original Lyrics of the song *****

    rote rote hasanaa sikho, hasate hasate ronaa
    jitanee chaabee bharee raam ne, utanaa chale khilaunaa

    hum do yek humaaree, pyaaree pyaaree muniyaa hain
    bas yahee chhotee see apanee saaree duniyaan hain
    khushiyon se aabaad hain, apane ghar kaa konaa konaa

    badee badee khushiyaan hai, chhotee chhotee baaton mein
    nanhe munne taare jaise, lanbee raaton mein
    ayesaa sundar hain ye jeewan jaise koee sapan salonaa

    mausam badale to mat dar jaanaa, gudeeyaan raanee
    saawan mein bijalee chamakegee, barasegaa paanee
    dharatee anbar bheeg jaaye, nainon ko naheen bhigonaa


    ******* Translation to the best of my understanding ******

    Don’t cry, learn to laugh and when laughing don’t cry
    The toy will move only as much as you wind its keys

    We are a couple and we have a very sweet daughter
    the small one means the whole world to us
    All the corners of our house are filled with happiness

    there is lots of happiness in small small matters
    just like millions of small stars in a long night
    like a dream such wonderful is our life

    My dearest daughter don’t get scared when the weather changes
    Thunder and lightning, rain will fall
    The earth will get wet but don’t wet your eyes

    ReplyDelete

  5. ee bwana umenikumubusha ticket mbu drive in msasani nilishawahi kuruka ukuta nikadakwa na walinzi the outcome was not good nashukuru kwani hatukuishia oysterbay polisi.
    kwa kweli ile miogo iliyokuwa ikichomwa pale drive inn ilikuwa na utamu wa aina yake huku pembeni ukiwa na mtafasiri wako anayekudanganya huku naye anajua kuwa anakudanyanga lakini unamsikiliza hivyo kusogeza masaa.

    ReplyDelete
  6. Nina kumbuka Ladies Show kila Jumamosi na Jumapili sa nane mchana.Asante.

    ReplyDelete
  7. Ankal umenikumbusha mbali wakati huo kuipata ticket ya movie mpya ilikuwa mbinde inabidi uwe na msuli otherwise utainunua bei mara mbili. wauzaji wakubwa wa ticket wakati huo kina Masanga, Raja kaka, Gashu, Kibonge na wengi wengine duh!!! kweli tumetoka mbali.
    Mdau Min zaman.

    ReplyDelete
  8. I can't believe you chose to show Amitabh Bachchan...Asante Bwana Michuzi

    ReplyDelete
  9. YEH DOSTI- SHOLAY WAS MY FAVOURITE, ACTUALLY SHOLAY IS MY BEST MOVIE EVER!

    ReplyDelete
  10. Mzee hiyo inanikumbusha mbali sana Enzi hizo Kule Metropol Arusha haiku na hata kwenda Sunday school

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...