Luton Tanzanian Community (LTC) Uingereza Kwa
kushirikiana na Tripple EM Inawaletea Sherehe za Uhuru wa Tanzania na Kenya
(Double Celebrations in one) Jumamosi Tarehe 15/12/2012, Roman Way Tomlinson Avenue LU4 0QL - Luton .
Kutakuwa na burudani za kumwaga vichekesho na majonjo
ya asilia yetu wana East African Nyama Choma, Tusker na Vyakula asilia vya
nyumbani km. Ugali, Kienyeji, Mihogo ya Kuchoma chachandu na Samaki n.k
Kiingilio ni Paundi tano tu kabla ya saa sita usiku na baada ya hapo ni Paundi
kumi.
Magoma yote ya mwambao na bongo flava na Mayenu kama
kawa chini ya ma DJs CYMOH, DJs PAPS, DJs JOE HAMEL na Mtaalam DJs Double T
wataangusha magoma kuanzia saa mbili usiku mpaka Majogoo Pia kutakuwa na
suprises kubwa ya kutisha siku hiyo usikose.
Watanzania na Wakenya wote UK bila kusahau wana Afrika
mashariki wote na marafiki Mnakaribishwa:
Abraham Sangiwa
Katibu - Luton
Tanzanian Community.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...