Ndugu wapendwa:
Kwa niaba ya ndugu yetu Richard Mwandemani
(DJ Rich Maka) familia yake, ndugu na jamaa, tunapenda kutoa shukran zetu za dhati kwa ushirikiano mwema
mliouonyesha toka mzee wetu Edson Mwandemani alipokuwa amelazwa hospitali kwa
kuja kumjulia hali hadi kilio
kilipotokea jinsi mlivyoshughulika kwa
misaada yenu ya hali na mali.
Hatuna cha kuwalipa ila Mwenyezi Mungu mwenyewe
atawalipa malipo yalio stahili.
Mwili wa marehemu mzee Mwandemani utaondoka
Ijumaa tarehe 28 December, 2012 kwa safari ya kwenda nyumbani na kufika
Tanzania Jumapili jioni December 30,
2012.
Asanteni sana na shukran kwa wema na
ukarimu wetu.
Isaac Kibodya, kwa niaba ya Richard
Mwandemani (DJ Rich Maka) na familia
yake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...