Kampuni ya Lakeland Africa ya jiji Dar es Salaam imeandaa safari ya kutembelea hifadhi za taifa na makumbusho ya taifa ili kutoa fursa kwa Watanzania kusherehekea msimu huu wa Krismas na Mwaka mpya.
Watanzania wanahamasishwa kujitokeza kushiriki katika safari hiyo ya kitalii ya siku 14 itakayoanza jumamosi ya Desemba 14 mwaka huu hadi Desemba 27 mwaka huu.
“Kwako mtanzania sasa inawezekana kujua Tanzania yako, si lazima kuwa mzungu kuwa mtalii wa ndani”
“Kwako mtanzania sasa inawezekana kujua Tanzania yako, si lazima kuwa mzungu kuwa mtalii wa ndani”
Safari hii itaanzia Dar es Salaam, na kupita katika hifadhi za Sadan, Pangani, Lushoto, Tarangire, Ziwa Manyara, Ngorongoro Crater, Hifadhi ya Serengeti na itahitimishwa Butiama kwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Safari hii itatumia magari ya kisasa makubwa yenye uwezo wa kubebe watalii 24 na kutoa nafasi kutumia vifaa vya umeme (laptop, simu, kamera) kwa kila mtalii kuwa na soketi yake.
Magari ambayo yamekuwa yakitumiwa na makampuni ya utalii katika nchi za ulaya sasa kutumika Tanzania pia.
Magari ambayo yamekuwa yakitumiwa na makampuni ya utalii katika nchi za ulaya sasa kutumika Tanzania pia.
Gharama za safari hii zinajumuisha chakula, malazi, usafiri, tozo za kuingia hifadhini na tiketi ya ndege kutoka Mwanza kurudi Nyumbani.
Kwa mawasiliano na Lakeland Africa
+255222-761811
+255784885901
Email: reservations@lakelandafrica.com
‘Kuwa mtalii ndani ya nchi yako’
Kwa kweli nawapa hongera kwa ubunifu huu HONGERENI SANA. Ushauri wangu je haiwezekani mkaanza na safari fupi fupi za kuishia let say mikumi na mikoa ya karibu ili mtu ajipange na familia au watoto tu kwa sababu wengi sasa wako likizo.
ReplyDeleteHii ni fursa pekee mkawa na mtu anayetoka TANAPA au kwenye vyuo vikuu mkashirikiana ili wanafunzi watakaotembelea hifadhi hizo wapate ufahamu wa kuipenda sekta ya utalii na hatimaye wajiunge kwenye vyuo na kuchukua masomo ya Tourism. ASANTE
Tunaomba watuwekee hapa gharama kabisa badala ya kuanza kupiga simu au kuandika email. Asante.
ReplyDeleteAsanteni sana LAKELAND AFRICA,
ReplyDeleteHuu ndio Uzalendo wa kuwapa mwamko wananchi wa kawaida kuijua hazina kubwa ya rasilimali ya Utalii nchini!
Shime Kampuni lukuki zilizopo nchini tuangalie na upande wa pili wa sarafu kwa Utalii wa ndani badala ya kuegemea kwa wageni Wazungu pekee!
HEKO LANDLAND AFRICA!
ReplyDeleteMmetoa mwelekeo na somo jipya kwa Wadau wa sekta ya Utalii nchini.
Ni mwanzo nzuri sana!
ReplyDeleteYaliwahi kumkuta jamaa yangu siku moja miaka ya 2005 aliamua kwenda Kanda ya Kaskazini Arusha akafikia Hoteli moja maarufu ya Kitalii pale.
Siku iliyofuata alidamka asubuhi akashuka floor ya chini Hotelini kwenye Kampuni moja ya kukodisha magari wa Mbugani, alipofika pale kwa kuwa alikuwa ni Mswahili wafanyakazi walimpuuza sana, kila mmoja alifanya lake, wakaja Wazungu wakapokelewa kama Wafalme!
Haikutosha jamaa akaulizia, wale wafanyakazi wakaendelea kumpuuza tena ajabu ni kuwa akatoa pesa kamili baada ya kutajiwa gharama kwa idadi ya siku atakazotumia gari na wasaidizi, isitoshe kila Msaidizi akawa anamkwepa anataka apangiwe na wageni Wazungu!
Baadaye akaja Bosi wao ambaye anajua kuwa jamaa anazo, akamkaribisha na ndio jamaa wafanyakazi wakazinduka.
Mwisho wa mambo wakajikuta wanapewa Tipu zaidi ya pesa wanazopewa na wageni Wazungu!
Safari ingine mwaka 2007 akaenda tena safari alipofika walikuwa wamemsoma naye akapokelewa kama Mzungu!
Wajameni hiyo ndiyo hali halisi anavyochukuliwa Mtalii wa ndani akifika sehemu za huduma!
Jamaa mmoja ambaye ni mmiliki wa Radio mahiri hapo bongo, aliniita mimi najifanya mzungu nilivyoenda na familia yangu mbugani serengeti, mimi nilimuita yeye ignorant na backwards.Kama mmiliki wa Radio ilibidi avalie njuga na kupiga debe suala la utalii wa ndani.Watu mjinyime bia and kiti moto muende kuifaidi nchi yenu mipingo!
ReplyDeleteMdau Ughaibuni.
Utalii wa ndani kwa huu mpango Wakonongo wengi nchini wanachukulia ni anasa !
ReplyDeleteWakati kama unatembea kwa safari hii unaweza kupata tiba ya Kisaikolojia kwa kushusha chini viwango vya Presha na Kisukari kiurahisi baada ya ziara hiyo!
Badala ya kujidunga sindano kila siku.