WAZIRI WA FEDHA MH. DKT. WILLIAM MGIMWA (MB) JANA IJUMAA 14/12/2012 ALIKUWA MGENI RASMI KATIKA UZINDUZI NA MAHAFALI YA KWANZA YA CHUO CHA MIPANGO YA MAENDELEO VIJIJINI,KITUO CHA KANDA YA ZIWA MWANZA.
KITUO HIKI KILIANZA KAZI RASMI TAREHE 25/09/2011 KIKIWA NA JUMLA YA WANAFUNZI 323 WALIOKUWA WAKISOMA MASOMO YA CHETI CHA MIPANGO YA MAENDELEO VIJIJINI AMBAPO JANA TAREHE 14/12/2012 JUMLA YA WANAFUNZI 269 WAMETUNUKIWA TUZO YA CHETI CHA MIPANGO YA MAENDELEO VIJIJINI.
AIDHA IDADI KUBWA YA WANAFUNZI HAO WAMECHAGULIWA KUENDELEA NA MASOMO YA ASTASHAHADA YA MIPANGO YA MAENDELEO KATIKA MWAKA WA MASOMO 2012/2013.
KITUO CHA KANDA YA ZIWA KIPO JIJINI MWANZA ENEO LA BWIRU PRESS NA NI TAWI LA KWANZA LA CHUO CHA MIPANGO YA MAENDELEO VIJIJINI KIPO DODOMA NA KWA SASA KINA WANAFUNZI 422 WANASOMA NGAZI YA CHETI NA WANAFUNZI 251 WANAOSOMA NGAZI YA ASTASHAHADA.
KATIKA SHEREHE HIZI MGENI RASMI DKT. WILLIAM MGIMWA ALIANZA NA KUZINDUA RASMI KITUO HIKI NA BAADAE KUWATUNUKU WANAFUNZI 269 TUZO YA CHETI KATIKA MIPANGO YA MAENDELEO VIJIJIJINI.
Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha,Dkt. William Mgimwa akiwa na Mkuu wa Chuo cha Mipango,Constantine Lifurilo.
kutoka kushoto ni Dkt. F.G.H Hawassi - Mkurugenzi wa Chuo cha Mipango Kanda ya Ziwa, Bw. Constantine Lifurilo - Mkuu wa Chuo cha Mipango Dodoma, Mh.Dkt Mgimwa na Dkt. Razack Lokina Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi.
wahitimu.
Mgeni Rasmi akipata maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na chuo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...