Mkuu wa udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bw.Kelvin Twissa,akionesha moja ya simu aina ya Nokia ambazo zitakuwa zikishindanishwa katika shindano litakalomuwezesha mteja atakayenunua simu ya aina hiyo katika msimu huu wa sikukuu kujishindia zawadi mbalimbali, pamoja na kupata fursa ya kuingia kwenye droo kuu,katikati Meneja Masoko wa Nokia Ellen Lupilli na Mkuu wa kitengo cha vifaa vya mawasiliano na wateja wa Vodacom Mgopelinyi Kiwanga.
Meneja Masoko wa Nokia Ellen Lupilli katikati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ofa za simu aina ya Nokia ambapo mteja atakaenunua katika msimu huu wa sikukuu atajishindia zawadi mbalimbali, pamoja na kupata fursa ya kuingia kwenye droo kuu,anaeshuhudia kushoto ni Mkuu wa Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bw.Kelvin Twissa na Mkuu wa kitengo cha vifaa vya mawasiliano na wateja wa Vodacom Mgopelinyi Kiwanga.
Wakati shamrashamra za maandalizi ya msimu wa sikukuu za mwishoni mwa mwaka yakiwa yanaendelea, Kampuni ya Vodacom Tanzania na Nokia zimetambulisha ofa kabambe kukamlisha furaha ya kuelekea kufunga mwaka wa 2012.
Kampuni hizo kwa pamoja zimezindua rasmi shindano litakalomuwezesha mteja yeyote atakayenunua simu ya mkononi aina ya Nokia, kujishindia zawadi mbalimbali papo kwa hapo, pamoja na kupata fursa ya kuingia kwenye droo kuu.
Mteja atakayenunua simu ya Nokia na kisha kuweka muda wa maongezi wa aidha Tsh 1,000 au Tsh 1,500 atapata kifurushi cha BURE chenye muda wa maongezi wa dakika 10, SMS 50 na internet ya MB10 kila siku kwa muda wa wiki moja.
Kila simu ya Nokia itakayonunuliwa itakua na namba maalumu/kuponi ambayo mteja atatakiwa kutuma namba hiyo kwa SMS kwenda 15544 ili kuingizwa kwenye droo. Kila SMS itakayotumwa kwenda kwenye namba 15544 itatozwa gharama ya kawaida ya SMS.
Washimdi wa droo hizo zitakazokuwa zikichezeshwa kila siku watakuwa wakijishindia zawadi za simu, chargers, t-shirts na headphones zitakazotolewa kwa wateja kama zawadi za papo hapo.
"Ushiriki wa kubahatika kujishindia zawadi za papo hapo humuwezesha mteja kuingia moja kwa moja katika Droo kubwa ya mwisho itakayofanyika Januari 11, 2013 ambapo washindi watapata simu za kisasa za Nokia Lumia."Alisema Mkuu wa Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa.
Washindi wa zawadi za kila siku watachukua zawadi zao katika maduka ya Vodacom yaliyochaguliwa, ambapo watapatiwa huduma stahiki.
Shindano hilo litafikia tamati ifikapo Januari 10, 2013, majira ya usiku, na Januari 11, 2012 ndiyo siku ambayo Vodacom na Nokia zitachezesha droo itakayoshirikisha washiriki wote wa shindano hili toka mwanzo, na kati yao mshindi atatangazwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...