Kuna nafasi ya kazi maalumu kwa ajili ya Mtaalamu wa Kuandika Tenders za namna mbalimbali regardless ni katika Sector gani. Kazi atakazofanya ni pamoja na:
1. Kuandika Tenders za Serikalini na Mashirika ya Umma kutegemeana na ToR
2. Kuandika Tenders na Proposals za Makampuni Binafsi
3. Kuandika Company Profile na kutafuta kazi
4. Kushiriki katika kufanya kazi zilizopatikana kama coordinator
5. Kuwasiliana na Ma-Consultants mbalimbali walioko katika database kwa kazi zilizopatikana
6. Kumaintain database ya Ma-Consultants mbalimbali
7. N.k.
Sifa Za Mwombaji:
1. Awe na Elimu ya Chuo Kikuu
2. Awe na utaalamu wa kuandika Tenders za aina mbalimbali kutegemeana na ToR
3. Awe na uwezo wa kufuatilia kazi mbalimbali: Sales & Marketing
4. Awe ana bidii ya kazi na mwenye kujituma
5. Awe anaielewa vema lugha ya Kiingereza: Kuongea na kuandika
6. Awe anajua kutumia vema computer na kuandika reports mfano: Ms-Word; Excel etc.
Mshahara utazingatia sifa za mwombaji.
Tuma maombi yako na CV haraka kwenda Mtsimbe@gmail.com & sam@danimex.com
Kweli tunakoenda sasa Tanzania yetu ni kubaya..ina maana hao walioajiriwa serikalini hawakusomea mambo hayo??au serikali haina wataalaam wanaoajiriwa katika vitengo wakiwa na taaluma za kuandika Tenders??
ReplyDeletemaana kwa sasa kuna watu hadi wanaadika thesis za watu..watu wako maalumu kwa kuandika reports mbalimbali za wanafunzi wa vyuo...
kweli tutafika kwa hali hii???
Sifa za Mwombaji:
ReplyDeleteSifa No.1
Awe na Elimu ya Chuo Kukuu
Haya sasa Waheshimiwa je kwa waombaji ambao wana uzoefu mkubwa sana na ujuzi wa Kazi hiyo ya kuandika Tenda ambao hawana sifa No.1 ina maana hawafai?
Uzeoefu unategemeana na kiwango cha Elimu?
Vigezo vya namna hii mara zote ndio vinakwamisha maendeleo ya Taaluma nchini, kwa kuwa uwezo wa kuandika Tenda hautegemei kiwango cha Elimu bali unategemea uzoefu na (CV), yaani kazi za Tenda alizofanikisha Mwombaji hapo awali.
PIA NI MUHIMU IELEWEKE YA KUWA HAKUNA KIWANDA AMA SAYANSI YA MIUJIZA INAYOZALISHA WAFANISI WA KAZI, BALI MFANISI WA KAZI ANATENGENEZWA NA MAZINGIRA NA USHIRIKISHWAJI KTK SEHEMU YA KAZI.
Vigezo kama hivi mara zote unakuta kwenye Mabango na Matangazo ya Ajira unakuta kazi inatangazwa Mwombaji anatakiwa awe na sifa hizi:
(i)Umri usio chini ya Miaka 35,
(ii)Uzoefu usiopungua miaka mitano (5)
(iii)Awe ameshafanya kazi hiyo ktk Taasisi zisizo 3 kwa miaka hiyo mitano akiwa hana rekodi mbaya ya kazi.
Sasa hebu tuangalie ktk rika la watafuta ajira walio wengi ambao ni Wahitimu wa Shahada mbalimbali ktk Elimu ya juu unakuta hawazezi kutimiza vigezo hivyo (i),(ii) na (iii) hapo juu!
Siyo tenda ni zabuni.
ReplyDelete