Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu kifungo cha miaka tatu jela mtu aliyedaiwa kumuibia Sh milioni 37 Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ally Hassan Mwinyi.

Mshitakiwa huyo ni Abdallah Mzombe ambaye amehukumiwa baada ya kumkuta  na hatia. Mbali ya adhabu hiyo, Mahakama imeamuru mshitakiwa kulipa fedha hizo wakati akitumikia kifungo hicho.

Hakimu Genvitus Dudu alitoa adhabu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka ambao ulikuwa na mashahidi saba.

Mshitakiwa huyo alikuwa anadaiwa kuiba fedha hizo baada ya kuaminiwa na Mwinyi kusimamia na kukusanya kodi ya nyumba zake mbili zilizopo Mikocheni B na Msasani jijini Dar es Salaam.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Dudu alisema, mshitakiwa amepatika na hatia ya makosa mawili ya wizi wa kuaminiwa,na anahukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kila kosa lakini atatumikia vifungo hivyo kwa wakati mmoja ambapo ni sawa na miaka mitatu.

kwa mujibu wa ushahidi mshitakiwa haibishaniwi alikuwa wakala wa kukusanya kodi katika nyumba za Mwinyi na alipokea fedha za kodi kutoka kwa wapangaji.


Katika makubaliano yao Mwinyi alimwambia Mzombe akipokea kodi, fedha nyingine afanye ukarabati wa nyumba hizo na nyingine fedha zinazobaki ampelekee lakini mshitakiwa hakufanya hivyo badala yake alizitumia kwa matumizi yake binafsi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa


  1. RUNDIKA MBWEHA HUYO!

    ReplyDelete
  2. Ndiyo tatizo letu Wabongo, jamaa labda alimpigia mahesabu Mzee Mwinyi, akifikiri si kiongozi mmstaafu, basi ana hela kibao na hata nikimdhurumu hamna neno au nitaenda kuomba msamaha tu halafu ataniachia. Hii iwe fundisho kwa wote wale matapeli, mtu anapokuamini na mali au mtaji wake fanya kile unachotakiwa kufanya, tuwe waaminifu. Kwa tabia ya uaminifu labda unaweza bahatika na wewe unatokea hapo hapo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...