Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi katika kikao chake cha siku mbili Februari 10 na 11, 2013 kilichofanyika mjini Dodoma, pamoja na mambo mengine kimeridhia uteuzi na kufanya uchaguzi wa Wajumbe 14 wa Kamati Kuu yake.

Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imeridhia uteuzi wa Dokta Salim Ahmed Salim kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu kupitia nafasi 10 za uteuzi wa Mwenyekiti wa CCM. 

Wajumbe 14 waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ni:-

Wajumbe wa Kamati Kuu - Bara
1. Ndugu Pindi Chana
2. Ndugu Adam Kimbisa
3. Ndugu William Lukuvi
4. Dokta Emmanuel Nchimbi
5. Ndugu Jerry Slaa
6. Profesa Anna Tibaijuka
7. Ndugu Stephen Wassira

Wajumbe wa Kamati Kuu - Zanzibar.
1. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha
2. Ndugu Hussein Mwinyi
3. Profesa Makame Mbarawa Mnyaa
4. Dokta Salim Ahmed Salim
5. Ndugu Maua Daftari.
6. Ndugu Samia Suluhu Hassan
7. Ndugu Hadija H. Aboud

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

 1. Kwa anayekumbuka somo la SIASA vizuri,kazi yao nini hawa hadi iwe Breaking News??

  David V

  ReplyDelete
 2. huu ndo muungano mzuri, usawa wa nchi.

  siyo eti kwa sababu zenji ni ukubwa wa wilaya ya bara basi wapate mtu mooja tuu.

  nyanya kubwa na ndogo zote nzima, hakuna sehemu.

  Nyanya ndogo ni bora zaidi ya kipande cha nyanya kubwa.

  ReplyDelete
 3. Hongera CCM kwa idadi sawa ya Wajumbe!

  Bara 7 na Visiwani 7.

  Je, Wapinga Muungano mmeona hiyo?

  ReplyDelete
 4. Ina maana idadi ya Wana CCM Bara na Zanzibar ni Sawa? Kigezo gani kinatumika kwa huu uwiano? Hapa Wabara tukilalamika tunaumizwa itakubalika?

  ReplyDelete
 5. WAJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM TAIFA WANAWAKILISHA KIZAZI CHA WAKATI HUU NA UJAO.

  TAFADHALI TUKISAIDIE CHAMA CHA MAPINDUZI KUFANYA MAAMUZI MAGUMU YANAYOTEKELEZEKA MAANA USHINDANI WETU NI DHIDI YA KERO ZA MAISHA YA WATANZANIA WOTE.

  MAPINDUZI SI LELE MAMA.

  MAINA OWINO.
  UK

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...