CHAMA cha mpira miguu Dar es Salaam(DRFA),
kimejipanga kukutana na wanachama wake wa mkoa huu, ili kujua kiundani jinsi
wanavyoendesha shughuli zao, kwa maana ya ufanisi, mikakati yao, chang’amoto
walizonazo na nini kifanyike ili matarajio yanayokusidiwa yafike kwa wakati
mwafaka.
Uongozi mpya tuliongia madarakani Desemba mwaka
jana, tuna kila sababu ya kufanya yale ambayo kila mmoja wetu alidhamiria
katika sera zake za kujinadi, hivyo hatuwezi kukurupuka, bila kwanza kukutana
moja kwa moja na wanaoguswa na changamoto mbalimbali za uendelezaji soka mkoani
Dar es Salaam na kuona ni jinsi gani DRFA inaweza kusaidia au kuchangia
maendeleo na utatuzi wa changamoto mbalimbali.
Katika mkakati huo, Februari 8, tutakutana na
chama cha waamuzi mkoani(FRAT Dsm), kujadili kwa kina idara yao na changamoto
zake kwani wao ni watu muhimu sana katika kufikisha dhamira za kweli ya
uendelazaji wa mchezo huu mkoani kwetu. Februari 9, DRFA itakutana na viongozi
wa chama cha soka wilayani Ilala(IDFA), pia kwa makusudio hayohayo.
Chama cha soka wilayani Kinondoni (KIFA), siku
yao itakuwa Februari 10 na ratiba hiyo itaendelea kwa vyama vingine shiriki
kadri tutakavyo panga. Vyama hivyo ni pamoja na Chama cha Soka la Wanawake
(DWFA) sanjari na Chama cha Mpira miguu wilayani Temeke (TEFA), ambao
hawajajibu wito wetu, lakini iwapo tu watafanya hivyo, kutakuwa na kikao nao.
Februari 12 mwaka huu, kutakuwa na kikao cha
pili cha kamati ya utendaji, pamoja na mambo mengine kupokea taarifa za
mikutano yote ya wadau tuliokutana nao na kuangalia nini kifanyike kwa maslahi
ya soka la Dar es Salaam.
Tunatanguliza shukrani
Msanifu Kondo.
Katibu Mkuu DRFA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...