Hoyce Temu akimpa mkono wa pole mke wa Marehemu Daudi Mwangosi alipoitembelea familia hiyo kuifariji.
Mwanaharakati wa kijamii Hoyce Temu kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania amefanya ziara mkoani Iringa na kupitia nyumbani kwa familia ya mwandishi aliyeuawa Daudi Mwangosi na kuwajulia hali.
Hoyce Temu kwa pamoja na kundi zima la waandaaji wa kipindi cha mimi ni Tanzania waliwasili katika nyumba ya mjane huyo Bi. Itika Mwangosi kumsabahi na kutaka kujua anaendeleaje na maisha kila siku.
Hoyce Temu akimfariji mke wa Marehemu Daudi Mwangosi Bi. Itika Mwangosi alipoitembelea familia hiyo mkoani Iringa.
Ziara hiyo nyumbani hapo ni kwa nia nzuri ya kutaka kujua jinsi anavyokabiliana na changamoto za kila siku za maisha pamoja na watoto wake wanne.
Walizungumza mengi yakiwemo yale yanayomkwaza Bi. Itika Mwangosi na jitihada anazofanya ili kujikwamua.
Aidha Bi. Temu akiwa amewapakata watoto wa marehemu aliifariji familia hiyo akiwataka kutokata tamaa na kuwa Mungu yupo na kwa kuwa watanzania ni wamoja mambo yatakwenda sawa.
Hoyce Temu akiwapa kumbatio la upendo watoto wa marehemu Daudi Mwangosi.
Bi. Itika Mwangosi akionyesha uso wa matumaini baada ya kupewa maeneo ya faraja na Hoyce Temu.
Amezungumza na watoto kuhusu kwenda shule na kutaka kujua wanasoma shule gani na iko umbali gani kutoka nyumbani.
Pamoja na mambo mengine Hoyce Temu kupitia kipindi cha Mimi na Tanzania amewasihi watanzania wenye moyo wa ukarimu kumsaidia Mjane huyo ambaye hana ajira kwa hivyo ni vigumu kupata kipato cha kujitosheleza yeye na wanawe kwa mahitaji muhimu ya kila siku.
Watoto wa Marehemu wakionyesha matumaini mapya baada ya kufarijiwa na Hoyce Temu.
Mtanzania mwenye ufariji kwa familia hiyo anaweza kutuma kiasi chochote cha fedha kwenye namba inayomilikiwa na mjane huyo Mama Itika Mwangosi kupitia mtandao wa M-Pesa: 0767670739 ili msaada huo uwafikie walengwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Acha kutonesha vidonda vya watu wewe.....

    ReplyDelete
  2. Kila nikijiweka nafasi yako dada Itika machozi yananitiririka ni vigumu mno kwako wakati huu kumpoteza mumeo aliyekua kila kitu. Ila usikate tamaa Mungu kamwe hawezi kukuacha.Kwani mumeo alienda kutafuta kama Mungu alivyomuamuru kwa jasho lake angekula. Tunakuombea upate faraja ya moyo na upone haraka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...