Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid akikabidhi zawadi ya trophy kwa Dkt. Yakiya kwa kutambua mchango 
  Dkt. Yakiya akiwa amepozi na zawadi yake,pichani kati ni  Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mnyaa Mbalawa, 
  Mkurugenzi Mkuu wa IAEA, Dkt. Yakiya Amano akitoa hotuba yake kwa wageni waalikwa
 Wageni waalikwa wakimsikiliza Dkt. Yakiya Amano, Mkurugenzi Mkuu wa IAEA katika ukumbi wa TFDA Makao makuu
  Mchunguzi wa Chakula katika maabara Bw. Rajab Mziray akitoa maelezo kwa Dkt. Yakiya na wageni wengine katika maabara ya chakula 
  Mtaalamu wa uchunguzi wa dawa Bw. Yonah Hebron akitoa maelezo kuhusu uchunguzi wa dawa  katika maabara ya TFDA kwa Dkt. Yakiya na wageni wengine
Mkurugenzi Mkuu wa TFDA akimwongoza Dkt. Yakiya pamoja na wageni wengine kuelekea maabara ya TFDA

======== =====  ==========

Ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Atomik Dr. Yukiya Amano kwa TFDA

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Atomik (IAEA), Dkt. Yukiya Amano, amesifu kazi nzuri inayofanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) katika udhibiti wa bidhaa za Chakula, Dawa, Vipodozi na Vifaa tiba katika Tanzania kwa lengo la kulinda afya ya wananchi.

Dkt. Yakiya Amano ambaye yupo katika ziara ya siku mbili nchini Tanzania, ametembelea TFDA kwa lengo la kujionea na kufuatilia utekelezaji wa miradi mbalimbali inayodhaminiwa na IAEA katika maabara ya TFDA.

Katika maelezo ya utangulizi, Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo, alieleza kuwa hadi sasa TFDA imekuwa ikitekeleza miradi miwili ya IAEA. Miradi hiyo ni URT 5024 ambao ulianza 2005 - 2009 ambapo TFDA ilipatiwa USD. 241,892 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya maabara na ukujengewa uwezo kwa wataalam wa Maabara. Kufuatia kujengewa uwezo na shirika la  IAEA, hivi sasa TFDA inachunguza sumu kuvu, kemikali za melamine na madini tembo kwa wastani wa sampuli  za 1000 kutoka 30 za mwaka 2008/09.

Sillo aliendelea kueleza kuwa, Mradi mwingine unaodhaminiwa na IAEA unajulikana kama RAF 5067 ulianza  Agosti 2012 utamalizika 2015 ambapo unajumuisha nchi 13 za Afrika ikiwepo Tanzania. Kupitia mradi huu, TFDA hadi sasa imepatiwa kifaa kiitwacho CHARM II cha thamani ya USD 55,015 na kemikali za thamani ya USD 6,637.

Akihutubia watumishi wa TFDA na viongozi wengine walioshiriki katika ziara hiyo, Dkt. Yakiya Amano aliwaeleza kuwa hivi sasa kumekuwepo na  ukuaji wa uchumi, idadi ya watu imeongezeka na mahitaji wa watu yameongezeka na hivyo kusababisha uwepo wa bidhaa nyingi katika soko lakini hata hivyo suala la usalama na ubora wa bidhaa za chakula na dawa havitaweza kuachwa bila udhibiti, hivyo udhibiti lazima uende sambamba na mabadiliko yanayotokea.

Dkt. Yakiya ameahidi kuendelea kushirikiana na TFDA katika kuhakikisha masuala ya udhibiti wa Usalama na Ubora wa bidhaa za Chakula, Dawa, Vipodozi na vifaa tiba yanapewa kipaumbele kwa lengo la kulinda wananchi.

Naye Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dr. Seif Rashid, katika hotuba yake ya kumkaribisha Mkurugenzi wa IAEA amepongeza ushirikiano uliopo baina ya Washirika wa maendeleo na TFDA na kusema kuwa mafanikio ya TFDA katika kulinda afya za wananchi yamechangiwa na wadau wa kimaendeleo ikiwa ni pamoja na IAEA.

Baada ya kutembelea Maabara ya TFDA, Dkt. Yakiya ameahidi kuisaidia TFDA katika kulipia gaharama za ufundi (USD 25,000) kwa mtaalam kutoka Kenya pamoja na ununuzi wa kifaa cha kupimia mabaki ya viuatilifu katika uchunguzi wa Chakula.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...