Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Urais wa TFF kabla ya kuenguliwa na kamati ya uchaguzi ya TFF,Jamal Malinzi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu hatua ya kuondolewa kwenye mchakato huo, ambapo alipinga kabisa hatua hiyo ya kuondolewa. Hata hivyo amemtaka Rais Tenga kumaliza vizuri kazi yake ambayo ameifanya kwa ufanisi wa hali ya juu kwa kulimaliza suala hili bila ya mgogoro zaidi.

Sababu zilizotolewa na kamati ya uchaguzi ya TFF ni uzoefu wa miaka mitano, Tuhuma za kupinga waraka wa kubadili katiba ya TFF baada ya kuwekewa Pingamizi iliyowekwa na Agape Fue ambaye, alikata rufaa kwenye kamati ya rufaa ya TFF kupinga kuto tendewa haki.

Alihoji kuwa huyo agape fue ni mwanamke au mwanaume kwasababu hajawahi kutokea kwenye kamati ya uchaguzi ya TFF wala kamati ya rufaa.
Waandishi wa habari mbalimbali waliojitokeza kwenye mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Naona dawa ni kuweka mgombea BINAFSI.

    ReplyDelete
  2. Kwa nini Mtu kulazimisha kuteuliwa uongozi? Hasa mtu anapokuwa na dosari za kiuongozi zilizo wazi??

    ReplyDelete
  3. Anony wa 02.44.00 pm hapo juu, hoja ni kwamba Bw. Jamal hana dosari yoyote ya kiuongozi kwa hiyo haikuwa sahihi kuenguliwa.

    ReplyDelete
  4. TENGA MBONA WAMALIZA KIPINDI CHAKO KWA KASHESHE?

    ReplyDelete
  5. WAKATI MALINZI AKIGOMBEA NA TENGA HAKUWA NA UZOEFU WA KUONGOZA?

    ReplyDelete
  6. TFF SI YA KUNDI LA WATU WACHACHE, HAKUNA HAJA YA KUPIGA KURA YA HAPANA NA NDIYO, HACHENI UDUKITETA

    ReplyDelete
  7. MSITUBURUZE NYIE TFF. MPAKA INAFIKA HATUA YA MWISHO KWELI HAMKUWEZA KIJUA KIPENGERE HICHO KAMA KILIKUWEPO NA KAMA MALIZI KINAMHUSU HUO NI UZEMBE TOSHA. KAMA MMESHINDWA HILO MNATUPA MASHAK

    ReplyDelete
  8. hapa mnadachezea nyau. TFF ni chama kikubwa sana na macho ya wa TZ yameangalia hapa kwa upande wa soka leo mnakuja na hoja ya danganya toto kwa masilahi yenu binafsi Tenga tatua jambo hili as soon as possible

    ReplyDelete
  9. Mdau wa nane (8) yeye Tenga ndio Fundi Mkuu wa matokeo haya sasa itakuwa ni vipi atalitatua hili?

    Yeye ndio aliyeweka 'Kura Turufu' hiyo !

    ReplyDelete
  10. Bongo kila kitu kime binafsishwa!

    Hadi Uongozi wa Chama cha Mpira u mikononi mwa Kundi la watu wanaohesabika licha ya nchi kuwa na watu zaidi ya 45 Mil.!

    ReplyDelete
  11. Tukumbuke Msemo usemao 'Ukipanda bangi utavuna bangi'

    'Ukipanda mchicha utavuna mchicha!

    Matokeo yake hapa ni kudumaa kwa Tasnia ya Soka nchini kwa kuwa Uendeshaji wa TFF na mchakato wa kuawapata viongozi ni wa Kimagomashi,,,hivyo kama tunapanda Magomashi tutegemee kuvuna magomashi kwenye maendeleo ya Michezo nchini.

    Uendeshwaji wa TFF na Mchakato mzima kuelekea Uchaguzi hauna tofauti na Genge la Mchezo wa Karata tatu!

    ReplyDelete
  12. Malinzi haijalishi hoja imeletwa na nani, unachotakiwa kufanya ni kujibu hoja ya pingamizi iliyopo mezani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...