Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Job Ndugai akitoa miongozo mbalimbali Bungeni leo.
Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo,Dkt. Fenella Mukangara akifafanua hoja ya Serikali ya Mfuko wa Mikopo kwa Vijana leo Bungeni mjini Dodoma.
Mbunge wa Ubungo,Mh. John Myika akiwasilisha hoja binafsi juu ya kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika jiji la Dar es salaam Bungeni leo.
wabunge wa upinzani wakiwa wamesimama wote kwa pamoja kupinga hoja leo Bungeni.

Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Tundu Lissu akitoka ndani ya ukumbi wa Bunge leo.
Naibu Spika Bunge,Mh. Job Ndugai (kulia) akionyeshwa makabrasha na Mbunge wa Arumeru Mashariki,Mh. Joshua Nassari muda mfui baada ya kuahurishwa kwa kikao cha Bunge leo.
Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Tundu Lissu (kulia} akijadiliana jambo na Naibu Spika wa Bunge,Mh. Job Ndugai nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo.Wengine ni Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Mh. Joshua Nassari na Mbunge wa Iringa Mjini,Mchungaji Msigwa.
Baadhi ya wabunge wakielekea ndani ya ukumbi wa Bunge leo Dodoma.picha na Mwanakombo Jumaa,Maelezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hawa wabunge wa upinzani wanadhani kupiga kelele na jazba ndo upinzani. Leteni hoja, upinzani sio ugonvi na vurugu jamani.

    ReplyDelete
  2. Ndilo tulilowatuma Bungeni nyie wabunge wa CCM? badala ya kututeteta ndio mmeamua kutuangamiza? Ole wenu 2015. Hamfai hata kidogo

    ReplyDelete
  3. Waheshimiwa wabunge, Spika na naibu wake, ningependa mtambue kwamba, sisi wananchi wa Tanzania tunaona, tunafuatilia kwa ukaribu sana kila kinachotokea hapo bungeni, tunasikitishwa na hatufurahishwa na mwendendo wa wabunge walio wengi kupuuza hoja za msingi ambazo ni kero kwa wananchi, kwasababu tu ya kuegemea chama fulani. Hatuna cha kufanya kwa sasa, lakini mtambue kwamba iko siku sauti zetu sitasikika, tumewatuma muende Dodoma kutuwakilisha, mtusemee, mtutee ili kero zinazotuzonga ziondoke, Je, hicho ndicho mifanyacho!!????

    ReplyDelete
  4. Msigeuze ubunge ni kazi ya kudumu, malizeni yaliyowapeleka mkafanye kazi za maendeleo/uzalishaji.

    ReplyDelete
  5. Mhe.Tundu Lissu kama KOMEDI!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...