Mfuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA} akikimbia kipigo alichokuwa akiangushiwa na wafuasi wa CCM katika eneo la uwanja wa wazi,karibu na barabara ya Mwanga mkoani Dodoma.Hii imetokea jana mchana wakati WanaCCM hao walipokuwa wanaadhimisha miaka 36 ya kazaliwa kwa chama Chao katika kata ya Uhuru, ambapo Wafuasi hao wa CHADEMA walienda katika viwanja hivyo na kuanza kuweka bendera yao sehemu hiyo huku shamrashara za wana ccm hao zikiwa bado zinaendelea.
mmoja wa wafuasi hao wa CHADEMA waliokamatwa katika sekeseke hilo akiwa ndani ya gari la polisi.
wafuasi wa CCM Wakimnyang'anya bendera ya Chadema mfuasi wa chama hicho aliyetaka kuiweka bendera hiyo sehemu ambayo ilikuwa inafanyikia sherehe ya maadhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM kata ya Uhuru mkoani Dodoma.
Bongo arosto.
ReplyDelete
ReplyDeletehahahhaha ni zaidi ya arosto nakwambia nimecheka balaaa
sasa huyo mtu wa chadema alifuata nini kunako CCM tena wangempiga afe kabisaaa sababu yeye ndo mgomvi nini kimempeleka huko wakati anajua kabisaa jamaa wako chali wanatafuta kujiokoa
hahahhahahah raha sana yaani hapo woote wajinga sio CCM sio CHADEMA hakuna mwenye afadhali wanatakiwa wapelekwe hapo milembe kupimwa akili
mhhh wabongo siku hizi wakali kama pilipili kichaa tunaposema vyama vya upinzani ndio huu wa kupigana? tuelimike wabongo tunatia aibu nchi za wenzetu upinzani wanashindania maendeleo ya nchi kujenga barabara usalama wa raia nyinyi mnagombea kitambaa cha kotoni kaaaaazi kweli kweli
ReplyDeleteAibu kubwa!
ReplyDeleteHuyu naye mpumbavu..huu ni uchokozi laivu...Chadema wasipoangalia watapoteza mwelekeo
ReplyDeletemkimuua mseme chadema wameanzisha fujo,.kwani kuweka bendera yake inawasumbua nini akilini? nyie si mmeshika mpini?au bado hamjiamini? acheni zenu hizo,na wote hapo mnaonekana wakimbiza mwenge tuu.ndio maana siipendi siasa.
ReplyDeleteHahahahaha!
ReplyDeleteHiyo 'move' au mwelekeo wa Wana CCM katika kumdhibiti Mwana Chadema ni mfano wa Wanasoka wanavyo gombea mpira wa kona ili kufunga Bao Golini!!!
Hapo mwenye Skafu Mgongoni kushoto ni Streka No.8, wa mbele yake mwenye Raba zenye stipu ya Puma ni Streka NO.9 na Mheshimiwa mwenye shati jeupe na suruali nyeusi kulia ni Streka No.10
Hapo Bao Wana-CCM halijamzamia Mwana CHADEMA?
Huo mshike mshike na saka nyoka alilofanyiwa Mwana Chdm hapo picha ya chini ni wazi akihojiwa ni rahisi kukubali kujiunga na CCM badala ya kuendelea kupokea Kipondo!
ReplyDeleteAma kweli Wana Chadema nyundo ya chuma yenye mpini wa chuma ya Chama cha Mapinduzi imewaangukia utosini mwa vichwa vyao!
ReplyDeleteMwana Chadema ni kama yupo mikononi mwa Mgambo wa RENAMO(Msumbiji) ama Mgambo wa UNITA(Angola)!
ReplyDeleteHapo ni Maamuzi ya Kundi yaani 'mob pschology' ambapo Maamuzi na adhabu ya chini kabisa kutoka kwa RENAMO/UNITA ni,,,kukatwa masikio kawoshi!!!
Picha ya chini mfuasi wa Chadema anajikuta yupo mikononi mwa Mgambo wa Frelimo ya Msumbiji!!!,,,hapo anapewa asaini Mikataba ya 'Nkomati'!
ReplyDeleteMara zote Mgambo wa Vyama vya Siasa wanakuwa na ghadhabu sana.
ReplyDeleteMfano kule Zimbwabwe, ZANU-PF ambayo ndio Chama Tawala waliendesha Kampeni moja ya kusimamia Eneo moja la Kijiji chenye Wafuasi wa chama pinzani eneo wanaloishi lisajiliwe kwa Makazi mapya ya Kisasa na Serikali.
Huku Wakazi wapinzani wasijue linaloendelea, eneo ile tu linasajiliwa, Mgambo wa ZANU-PF waliingia na michi na magongo usiku wa manane wakavunja majumba na kuwafanya jamaa wakakosa Makazi.
Kwa kuwa eneo lilisha sajiliwa kwa kuwa Makazi mapya na sio holela, Wapinzani walipoenda Mahakamani walishindwa Kesi!!!
WIMBO:
ReplyDeleteAmekoma, amekoma!
Kujitia tia kwake amekoma! X 5
Hivyo ndivyo atakavyosema Mwana CHDM baada ya uvamizi wake kwenye Sherehe za CCM.
Hivi wewe mwana Chadema hujui kuwa tarehe 5/2/1977 ilizaliwa CCM?
Hukuwa na taarifa ya kuwa CCM inasherehekea siku yao ya kuasisiwa chama?
Kwa nini usiulize Chadema kutaka kujua iliasisiwa tarehe ngapi ukafanye sherehe yenu?
Kwa kujichanganya kwake yeye mwenyewe Mwana Chadema anashuhudia akimezwa na mamba ndani ya Ngome ya CCM!
ReplyDeleteUlitakiwa kwa utaalamu wa Kijasusi uje hapo kimya kimya, tena bila Magwandazzz, loh ungefaidi sana tu!
Si umejitakia mwenyewe, wewe unajua upo Polisi halafu unachukua msokoto wako kibindoni unawasha kiberiti unawasha ganja?
Ukisikia Ushabiki maandazi ndio huo wako wewe Chadema.
ReplyDeleteSasa sherehe sio za chama chako wewe umefuata nini hapo?
Kama ungekuja kimya kimya yangekukuta hayo?
Unaona sasa? ukabebwa mzobe mzobe hata familia yako nyumbani ikiona picha hii utaaibika sana!
Kwa kweli kama Mdau hapo juu alivyosema, hawa wote ni wagonjwa!
ReplyDeletePana umuhimu Msajili wa Vyama vya Siasa akasisitiza kila chama cha Siasa kuwa na Taasisi ya kuwanoa Makada wa Chama na Wanachama juu ya Siasa zenye tija na ustaarabu.
Ni muhimu pia vyama vyote ili tupate maendeleo ya Kisiasa vikawa vinawekeza zaidi katika Mafunzo na Semina za siasa kwa Makada na Wanachama wake.
Hivi kwa Mtaji huu wa kukakamaliana tutafika kweli?
Heee hii ni Mieleka au ni Siasa?
ReplyDeleteAu jamaa wapo kwenye Komedi?
Inawezekana pia Michuzi amekosea jamaa wana ekti picha ya harakati za Siasa nini?,,,inawezekana wana SHUTI picha !
Hiyo peleka peleka ya hapo, twende twende inakuwa kama anasakwa Fisi maji msituni!
ReplyDeleteHizi Siasa za liede liende kweli tutakwenda na wakati?
Pana Political Integration protocol ktk hii Afrika ya Mashariki.
Si Wa Tanzania tutachekesha kwa wenzetu na aina yetu hii ya Siasa ya kupelekana resi resi?
Hiyo peleka peleka ya hapo, twende twende inakuwa kama anasakwa Fisi maji msituni!
ReplyDeleteHizi Siasa za liede liende kweli tutakwenda na wakati?
Pana Political Integration protocol ktk hii Afrika ya Mashariki.
Si Wa Tanzania tutachekesha kwa wenzetu na aina yetu hii ya Siasa ya kupelekana resi resi?
(hapa walikuwa wana ekiti video ya Leka Digutile)
ReplyDeleteUkisikia LEKA DIGUTILE ya Wanamuziki wa Kigoma wa wakiimba sambamba na Mhe.Zitto Kabwe ndio hiyooo!
Wa Majuu Madiaspora mmeona hiyo?
ReplyDeleteKushiriki Siasa kwa sasa unatakiwea uanzie kwenye Ubondia kwanza.
Siasa za Bongo ni MCHAKA MCHAKA!
Mwana Chadema ni wazi ataandika kumbukumbu kwenye Notebook yake kibindoni, tarehe, saa,sababu zilizopelekea yamkute na mahala yalipomkuta mambo!
ReplyDeleteAtapata kwa siku hiyo cha kuwahadithia wanawe na Mkewe nyumbani kwake!
Atapata cha kuja kuwasilimulia Wajukuu zake Uzeeni!
Mshike mshike alioupata kwa shari zote mwenyewe kutoka kwa wana CCM mchezo?
Purukushani inayofanywa baina ya Wanasiasa hapo (CCM na Chadema) inanikumbusha matukio haya mawili:
ReplyDelete1.Gari bovu linapo sukumwa ili liwake!
2.Ng'ombe hasa mkorofi anapokuwa Mnadani akipandishwa kwenye Lori kupelekwa Machinjioni!