Wazir wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa akionyeshwa Mfumo wa Maji Taka na Meneja Mazingira Bw Dominick Mariki wakati Waziri alipofanya Ziara ya Kutembelea Kiwanda cha Bia cha Serengeti Breweries cha Jijini Dar es Salaam ambacho Wananchi wanakilalamikia kinawamwagia Maji Machafu katika Mtaa wa Chamwenyewe Chang'ombe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Terezya Huvisa akimsikiliza Operesheni Meneja wa Kiwanda cha Bia cha Serengeti Shekhor Mokosare, Waziri alifanya Ziara ya kukagua na kuangalia Uchafuzi wa Mazingira Unaofanywa na Kiwanda cha Bia cha Serengeti cha Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa akimsikiliza Bi Mwaka Washokela kuhusu Malalamiko ya Umwagaji wa Maji Machafu ya Kiwanda cha Bia cha Serengeti katika Mtaa wa Chamwenyewe, Chang'ombe Jijini Dar es Salaam.Picha na Ali Meja
-
Wito umetolewa na Waziri wa Mazingira ofisi ya makamu wa Rais Bibi Terezya Huvisa kwa wenye viwanda na Hoteli za kitalii kote nchini kuzingatia usafi wa mazingira sababu mazingira ni uhai. Alitoa rai hiyo wakati wa ziara yake iliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa kutembelea baadhi ya viwanda na Hoteli za kitalii.
Viwanda alivyotembelea ni pamoja na Serengeti Breweries
Kiwanda kingine alichotembelea Waziri ni kiwanda cha kuchapisha maandishi kwenye fulana na vipeperushi ambacho kinaitwa CI Group kilikutwa na makosa mabalimbali ikiwamo uchafu wa mazingira ya kiwanda kwa ujumla, mazingira wanayofanyia kazi wafanyakazi wa kiwanda ni machafu sana hivyo kupelekea afya zao kuwa hatarini. Hata hivyo wamiliki wa kiwanda hicho walikimbia baada ya kumuona Waziri na ujumbe wake wakiwasili. Bibi Huvisa ametoa agizo kwa watu wa NEMC kwenda kukifunga kiwanda hicho mara moja.
Waziri Huvisa pia alitembelea hotel mbalimbali katika maeneo ya Oysterbay ambapo wameagizwa kuwasilisha cheti cha mazingira, na kama hawana hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwamo Hotel kufungwa.
Mwisho Waziri amewataka wenye Hotel kutilia mkazo swala zima la kutibu maji.
Seacriff, Golden Tulip, Police Mess na Coco beach nadhani zote zimekiuka sheria za mita 60 toka ufukweni. Coco ni ya walala hoi kwahiyo itafungwa tu,Police Mess ni serikali kwahiyo...., Seacriff na Golden tulip ni za wanene na uwekezaji mkubwa umewekwa na wahusika walikuwa wapi wakati zinajengwa. Si haki kufungwa wakati watu wahusika walisha bugi men. Sasa Slipway na double tree, mbalamwezi nk. itakuwaje.
ReplyDelete