Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (katikati) akikata utepe kwa kushirikiana na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la nguvu za Atomiki  Duniani Yukiya Amano (wa pili kutoka kushoto) kuashiria uzinduzi rasmi wa  jengo jipya lenye  vifaa vya kisasa kwa ajili ya  kuwahudumia wagonjwa wa kansa katika Taasisi ya Kansa Ocean Road jijini Dar es salaam. Wengine ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto), Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kansa Ocen Road Prof. Twalib Ngoma (wa tatu kutoka kushoto) na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Seif Rashid.
 Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (katikati) akiwaonyesha wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa jengo jipya la kuwahudumia wagonjwa wa kansa  katika Hospitali ya Kansa Ocean Road  kitabu cha Mkakati wa Kitaifa wa Kudhibiti na kupambana na Kansa nchini.
 Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la nguvu za Atomiki  Duniani Yukiya Amano akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  jijini Dar es salaam mara baada ya kuzinduliwa kwa jengo jipya la Taasisi ya Kansa Ocean Road lililojengwa na serikali ya Tanzania huku  shirika hilo likitoa msaada wa mashine mbili kwa za kutambua athari za ugonjwa wa kansa kwenye mwili wa binadamu.
 Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)  jijini Dar es salaam mara baada ya kuzindua jengo jipya la Taasisi ya Kansa Ocean Road lililojengwa na serikali ya Tanzania lenye uwezo wa kuhudumia wa 257 kwa gharama ya shilingi bilioni 7.2 huku Shirika la nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) likichangia mashine 2 za kutambua sehemu zilizoathiriwa na ugonjwa wa kansa katika mwili wa binadamu zenye uwezo wa kuhudumia wagonjwa 1600 kila moja kwa mwaka.
 Baadhi ya wataalam wa Taasisi ya Kansa ya Ocean Road  wakiwa ndani ya moja ya chumba cha  jengo jipya lililozinduliwa jijini Dar es salaam chenye moja ya mashine yenye uwezo wa kuwahudumia wagonjwa 1600 kwa mwaka. Mashine hiyo imetolewa na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA).
Sehemu ya nje ya jengo jipya la Taasisi ya Kansa ya Ocean Road lenye vifaa vya kisasa lilozinduliwa  jijini  Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Uchimbaji wa madini ya Urani uanoendelea huko Miradi ya Nantumbo na Mto Nkuju, kazi tunayo!

    Tusubiri Mionzi kwa Matibabu.

    ReplyDelete
  2. Bora maana Kansa TZ ilikuwa inatibiwa kidizaini na matibabu yaliyotumika mwaka 47. Tumshukuru Mungu kwa maendeleo hayo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...