Siku moja baada ya kamati ya rufaa ya shirikisho la soka nchini kumuengua mgombea urais wa TFF, Ndugu Jamal  Malinzi kutoka kwenye kugombea urais katika uchaguzi ujao wa TFF, leo hii wadau tofauti wa michezo wametoa maoni yao kuhusiana na sakata. Mmoja wa wadau aliyepaza sauti kuzungumzia suala hilo ni naibu wa waziri wa michezo, Bwana Amos Makalla (pichani shoto).

Akizungumza na Ibrahimu Masoud kupitia kipindi cha michezo cha Sports Extra cha Clouds FM jana  usiku, Makalla alisema ameshangazwa sana na kitendo cha kamati ya rufaa kumuengua Malinzi kwa sababu ambazo ameziita hazina mashiko na zimekosa ushawishi.

"Mimi kama mdau wa soka na michezo kwa ujumla napenda kusema kuhusu hili bila kupepesa macho kwamba kamati hii imepotoka kwenye suala hili. Hii kamati kwenye hili inataka kujishushua heshima, unajua wakati mwingine unaweza kujishushia heshima kwa gharama nyepesi. 

"Sababu walizotoa kumuengua Malinzi zimekosa ushawishi. Hoja walizotoa mimi kama mwanamichezo naona hazina mashiko. Malinzi anakosa vipi uzoefu sasa hivi, huku akiwa kiongozi wa chama cha soka cha mkoa? Alishawahi kuwa katibu wa klabu kubwa kama Yanga kwa miaka kadhaa, pia hi huyu huyu Malinzi ambaye aligombea urais wa TFF dhidi ya Tenga wakati huo, sasa iweje kipindi hicho aweze kugombea na sasa hivi ashindwe eti kisa kakosa uzoefu. Uzoefu gani wanauzungumzia ambao alikuwa nao kipindi hicho na asiwe nao sasa," aliongeza Naibu waziri huyo.

"Maamuzi ya namna hii yanadhoofisha kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya Mhe. Rais Jakaya Kikwete katika kurudisha uzalendo kwenye michezo. Rais amefanya mengi katika kuhamasisha watu kupenda michezo, sasa hivi watanzania tumeanza kupenda michezo. Tenga ameongoza vizuri na sasa tunahitaji TFF makini itakayokuwa ikiongozwa na viongozi makini watakaoiongoza soka yetu na hatimaye tuweze kwenda AFCON na World Cup.

"Mimi kama waziri wa Michezo ninamuomba Rais Tenga aliyewateua watu wa kamati hiyo aingilie suala na kuweka sawa, hali isije kuwa mbaya na watu wakaanza kupoteza upenzi na soka kwa mambo ya ajabu kama haya. Viongozi wa kamati kama walitaka tujue na madaraka na uwezo wa kufanya hili walilofanya wamefanikiwa kwa hilo, lakini sasa nawaomba watumie busara. Wasiwafanye watanzania waache kupenda mpira, wasiturudishe nyuma na jitihada za serikali katika kukuza michezo. Nawaomba wamrudishe Malinzi kura zipigwe kwa haki tupate uongozi bora." - alimaliza naibu waziri huyo wa michezo na utamaduni.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Watu wengine hapa nchini hawana umakini katika uongozi wa michezo na hii ni mojawapo wa sababu zinazodhoofisha michezo nchini! People are not serious!!

    ReplyDelete
  2. hongera waziri kwa kuliona hili

    ReplyDelete
  3. Tumechoshwa na tabia ya kuwaweka viongozi wote wa ngazi za juu TFF kuwa na uyanga yanga tunataka mabadiliko!

    ReplyDelete
  4. Mheshimiwa bwana..! Sasa sie kina yakhe tutasemeje??

    ReplyDelete
  5. Hoja za waziri zinanifanya nitilie shaka uwezo wake wa kufikiri na kupambanua mambo!

    ReplyDelete
  6. Sasa waziri mzima kuongea kwenye vyombo vya habari maana yake nini? Hajui mambo ya collective responsibility" Inabidi Kikwete amuwajibishe.

    ReplyDelete
  7. Kwa nafasi ya Urais hakuna mwenye uwezo wa kuongoza TFF si Nyamlani wala Malinzi. Nafasi itangazwe upya watu waombe tena.













    ReplyDelete
  8. Asante naibu waziri kwa kujulisha suala hili,nashauri Tenga awaite watu wake mapema

    ReplyDelete
  9. Hongera mheshimiwa kwa kingilia kati, hadi sasa nashangaa kusikia haya, siamini.hivi ni kweli nyamlani anasifa zaidi ya malinzi? Au manji anasifa gani zaidi ya malinzi! Mbona yeye kapita au wanataka pesa zake? Tunajua wanatafuta muovu wa kuwalinda na wizi wao

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...