Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa katika mazungumzo na Mhe. Yukiya Amano, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) alipofika kumtembelea Wizarani leo.
Mhe. Yukiya Amano, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani akifafanua masuala mbalimbali kuhusu Shirika hilo kwa  Mhe. Membe.
Mhe. Membe (kushoto) na Mhe. Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.), Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani, Mhe. Yukiya Amano (hayupo pichani) wakati akizungumza nao leo.
Mhe. Juma Duni Haji (kulia), Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,  Mhe. Dkt. Binilith Mahenge (katikati), Naibu Waziri wa Maji na Balozi Celestine Mushy (kushoto), Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani, Mhe. Yukiya Amano (hayupo pichani).
Mhe. Yukiya Amano (kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani akimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo yao leo. Wengine katika picha ni Prof. Manase Selema (katikati), Mkurugenzi wa Divisheni ya Ulaya ya Shirika hilo na Bw. Conleth Brady, Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu.
Mhe. Membe akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Yukiya Amano mara baada ya mazungumzo yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Huyu mgeni Bwana Mkuwa wa IAEA-International Atomic Energy Agency, anachotaka ni nini kimeandaliwa (SERA MHIMILI) ili kutoa Usalama wa afya za binaadamu , mazingira natahadhari za ziada kulingana na shughuli zauzalishaji zinavyoendelea kule Nantumbo Project na Nkuju River Project...(98U238)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...