Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo (aliyebeba mtoto) akiwa katika
picha ya pamoja na wanakikundi cha Nguvu Kazi pamoja na maofisa wa
Vodacom muda mfupi baada ya Mkuu huyo wa Wilaya kukabidhi mikopo nafuu
isiyo na riba wala dhamana kwa vikundi kumi vya wanwake wajasiriamali wa
kata ya Kwa mndolwa vyenye wanawake wajasriamali wadogowadogo zaidi ya
90. Mikopo hiyo imetolewa na Vodacom Foundation kupitia mradi wake wa
Mwei.
Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo akimsikiliza Meneja Uhusiano wa
nje wa Vodacom Salum Mwalim wakati wa hafla ya kuwapatia mikopo ya Mwei
wanawake wajasiriamali zaidi ya 90 wa Kijiji cha Kwa Mndolwa Wilayani
Korogwe.
Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon akiongea katika hafla ya
kuwapatia mikopo ya Mwei wanawake wajasiriamali zaidi ya 90 wa Kijiji
cha Kwa Mndolwa Wilayani Korogwe. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe
Mrisho Gambo na Meneja wa Uhusiano wa NJe wa Vodacom Salum Mwalim.
Mikopo hiyo isiyo na riba wala dhamana imetolewa kwa wanawawake hao
mwishoni mwa wiki kijijini hapo.
Akina mama wajasiriamali wa kata ya Kwa Mndolwa Wilayani Korogwe
wakimtumbuiza Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo(hayupo pichani)
muda mfupi baada ya Mkuu huyo wa Wilaya kuwasili katika kijiji cha Kwa
Mndolwa mwishoni mwa wiki kuongoza hafka ya kukabidhi mikopo nafuu kwa
wanawake zaidi ya 90 iliyotolewa na Vodacom Foundation kupitia mradi
wake wa Mwei
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo akiongea katika hafla ya
kuwapatia mikopo ya Mwei kutoka Vodacom Foundation wanawake
wajasiriamali zaidi ya 90 wa Kijiji cha Kwa Mndolwa Wilayani Korogwe.
Kushoto ni Meneja Uhusiano wa NJe wa Vodacom Salum Mwalim na Meneja wa
Vodacom Foundation Grace Lyon (Kulia). Mikopo hiyo isiyo na riba wala
dhamana imetolewa kwa wanawawake hao mwishoni mwa wiki kijijini hapo
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo akimkabidhi Hadija Tengeza wa
kijiji cha Kwa Mndolwa mkopo wa Mwei kutoka Vodacom Foundation
uliowanufaisha wanawake wajasariamali zaidi ya 90 wa kijijini hapo.
Wengine picha kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Tawala wa Korogwe Martha
Munuo, Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim, Afisa wa Vodacom
Foundation Ally Mbuyu na Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon(kulia).
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo (wa kwanza kushoto) na Meneja
Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim wakifuatilia maongezi na Meneja
wa Vodacom Foundation Grace Lyon(wa kwanza kulia) wakati Mkuu huyo na
msafara wake ukiwasili katika kijiji cha Kwa Mndolwa kuongoza hafla ya
utoaji mikopo ya Mwei mwishoni mwa wiki, Zaidi ya wanawake 90
wamenufaika na mikopo hiyo nafuu isiyo na riba wala dhamana.
Hongera Vodacom!
ReplyDeleteAma kweli mmewezesha saaana,
Yaani mtu asiyekopesheka mmemwamini na kumpatia!
Hii yataka moyo kwa kweli!!
Hii si ni sawa na Kumdhamini Teja ama mtu wa Mazishi?