habari za leo,

naomba uniwekee mada yangu kwenye mtandao wako.

Naomba kuuliza wizara ya elimu watueleweshe kuhusu maana ya michango ya ushirikishi shuleni kila siku. maana katika shule ya msingi Boko wilaya ya kinondoni imekuwa ni kero kwa watoto na wazazi watoto wanapigwa kwa ajili hilo mfano darasa la saba kila siku asubuhi ni lazima waende na sh. 300 na wanaambiwa ni lazima vinginevyo wanapigwa sasa nimepiga mahesabu kama watoto ni 300 kila siku kila kipindi kinakusanya sh. 300 x 300 = 90,000/= hizo hela zinaenda wapi. ukiuliza wazazi wanasema kwenye kikao cha shule walisema sio lazima  kwa hiyo aina maana mzazi asipompa mtoto hela lazima apigwe. Nawaomba Wizara ya Elimu watueleweshe kama ni kitega uchumi cha walimu? au inakuwaje?
Mdau 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Shule zote za kata wanafanya ufisadi huu. Shule ya Msingi Karume wanakusanya kwa watoto woooote wapatao 2000 kuanzia darasa la kwanza hadi 7. Tshs 300 kila siku. Jumamosi Tshs. 1,000/- eti Tuition. Ni unyanganyi Jua likiwaka. Hoja ya Elimu Bungeni ipewe kipao Mbele.Wabunge

    ReplyDelete
  2. HAWA WALIMU WANAWAFANYA WANAFUNZI KAMA KITEGA UCHUMI?KAMA MISHAHARA NI KIDOGO WALALAMIKIE WIZARA YA ELIMU NA SERIKALI SIO MNAWATESA WATOTO NA WAZAZI,MWALIMU MKUU ASHITAKIWE HARAKA SANA.TENA WARUDISHE PESA ZOTE KWA WATOTO.MDAU LONDON.

    ReplyDelete
  3. Jamani, sisi walimu hatuna posho za vikao kama nyie mnaokalia viti vya kuzunguka, mbona mnaingilia michongo ya watu?
    Mwalimu Kigamboni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...