Sina hakika sana ni wapi lakini mara ya mwisho nimeishika  nikiweka mafuta pale Total Petrol Station ya Mlimani City. Niliweka mafuta kisha nikalipa pesa. Nilipowaomba risiti yule muhudumu akaniomba nisogee mbele kidogo ningoje waniletee risiti maana kulikua na magari mengi kidogo yanatangoja huduma , hivyo nilisogeza mbele kidogo kisha nikapaki na ili kuokoa muda, nilishuka kumfuata aliyekua ananiletea risiti ili kuichukua. 

Sasa ninahisi nilipotoa pesa sikurudisha wallet mfukoni bali niliiweka juu ya mapaja na hivyo niliposhuka huenda niliingausha chini na sikugundua. Nimekuja kugundua tayari niko Ukonga nilipokuwa nakwenda. Nimejaribu kufuatilia sijaipata hadi sasa hivi. Ndani ya wallet kulikua na pesa si, vitambulisho, mastercards za bank tatu, leseni yangu ya udereva, kadi ya bima ya afya (green card), kitambulisho cha kazi na vitu vingine nisivyovikumbuka kwa haraka.

Business cards zilikua zimeniishia hivyo sina uhakika kama kuna kitu kilichokua na mawasiliano ya namna ya kunipata kama vile namba za simu. Kitambulisho changu cha kazi kinaonesha kuwa ni mwajirwa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mlimani.

Kwa atakayekuwa ameikota ninaomba na ninatanguliza shukurani zangu kwa kunisaidia kunipa vilivyomo.

Namba zangu za simu kwa ajili ya mawasiliano ni:  0782 581941 au 0 713 581941  au 0756 581941

AHSATENI.

Mathew Mndeme (MM)
Department of Computer Science and Engineering 
University of Dar es Salaam
P.O. Box 35062, Dar es Salaam.

Phone: +255 (0) 782 581941 / 713 581941 / 756 581941

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. How on earth would you have three mastercards? Would one not be enough with a certain limit? Pole sana mbongo!! I hope you do get your items back.

    ReplyDelete
  2. Go block ur number quick! getting this back is a brpbability!

    ReplyDelete
  3. Pole sana Mwalimu Mndeme jaribu kuulizia kituo cha polisi cha karibu na eneo la tukio mara nyingine vibaka hutupa karibu na vituo ili mwenyewe apate doc zake

    ReplyDelete
  4. Aise pole mkuu.Kama gari yako ina step(ubapa wa Kukanyaga wakati unapanda gari) utakuwa umeidondoshea barabarani ulipoonda hapo"SHELL",mara nyingi vitu vya kudondokwa kwenye gari vinadondoka hapo.Usiache kuangalia na kwenye gari humo chini/nyuma/pembeni ya kiti cha dereva,droo ya pembeni ya mlango wa dereva n.k.

    David V

    ReplyDelete
  5. mdau wa pili nini maana ya neno brpbability? tufunze nasi tuelimike tujuwe kusema kiingilishi.

    ReplyDelete
  6. Nawashukuru wote mulioniombea na kunitakia mafanikio. Mungu amekua mwaminifu nimeipata wallet pamoja na vyote vilivyokuwemo ipokua vijisenti ambavyo nadhani waluokota waliamua kujipongeza kama ujira wa kunihifadhia vingine..lol. Nimewashukuru na kumshukuru Mungu kwa uungwana wao pia kwani wangeweza kuvitupilia mbali

    Ni kweli kuwa niliangusha paleplae Petrol Station kwani waliookota wameikotea hapohapo nilipokua nahisi.

    Mungu awabariki

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...