Na Mahmoud Ahmad,Arusha

Akitangaza matokeo hayo jana mjini hapa rais wa taasisi iliyoandaa tuzo hiyo Dk. Phillip Imler wa Marekani mbele ya waziri mkuu Mizengo Pinda alisema sababu iliyopelekea Tanzania kupata ushindi huo ni kutokana na kuwa na vivutio vya kipekee.
Akielezea hifadhi ya taifa ya Serengeti alisema kuwa ndio hifadhi ya kipekee iliyopata kura nyingi na kutokana na tabia za misafara ya wanyama wanaohama kwa msimu maarufu kama annul animal migration.

Alisema kutokana na sifa ambayo Tanzania imezipata kupitia vivutio vyake vitatu itaendelea kuvitunza kuhakikisha kuwa vinavutia zaidi watalii na kuongeza pato la taifa.
“Afrika ina vivutio vingi vyenye kuvutia hivyo kila nchi ni lazima ijivunie rasilimali hizo kwa kuvitunza na kuviendeleza,”alisema
“Kwa Tanzania ni bahati ya pekee kwa kuweza kupata tuzo tatu za maajabu saba ya Afrika ambazo ni za Mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro pamoja na hifadhi ya Taifa ya Serengeti hivyo ni wajibu wa kuvitunza na kuviendeleza,”alisema Pinda.
Aliongezea kuwa iwapo watanzania wataendeleza tabia ya utunzaji wa vivutio vilivyopo nchini, nchi itaendelea kupata sifa duniani kote.
Naye Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa,(TANAPA),Dkt. Alan Kijazi alisema mlima Kilimanjaro ni mlima mrefu barani Afrika na hivyo una kila sababu ya kushinda na watanzania waendelee kuutunza.
Dkt Kijazi alisema kuwa hifadhi hiyo imeshinda kwa kuwa kuwa na wanyama wa kila aina kama Big Seven, Simba, tembo, Viboko, Nyati, Vifaru, Sokwe na Mamba.
.jpg)
Aidha Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki alisema ushindi huo ni historia kubwa duniani na kwamba ni jambo la watanzania wote kujivunia.
Pia aliwashukuru wananchi walioshiriki katika mchakato mzima wa kupiga kura na kuviwezesha kuingia katika ushindi kwa mara tatu.
ReplyDeleteS A L U T E ! ! !
KWA MANTIKI HIYO, TANZANIA INATAKIWA KUSHIKA NAFASI YA TATU KWA MAENDELEO YA KIUCHUMI BARANI AFRIKA.
ReplyDeleteNamshukuru muumba kwa kunipa nguvu na uwezo wa kutembelea sehemu zote tatu na nyingine pia.
ReplyDeleteHii ni fursa ya kuanza kujitangaza kabla hali haijapoa maana kuna msemo unasema MCHUZI WA MBWA UNANYWEWA UNGALI MOTO, tutabaki tunapongezana tunasahau majukumu ya kufanya promotion
ReplyDeleteHongereni sana watanzania wenzangu!
ReplyDeleteWATANZANIA TUNATAKIWA KUWA WATALII NCHINI MWETU LAKINI GARAMA ZIKO JUU SANA.BODI YA UTALII FANYIA HILO KAZI. MASHULE YAMEJITAHIDI KUPELEKA WANAFUNZI KUTALII LAKINI BADO WAZAZI INAKUWA NGUMU SANA KUKABILI GARAMA HIYO
ReplyDelete