Tanzania Commission for Universities
Notice to Public
TANZANIA BUSSINESS SCHOOL
Tanzania Commission for Universities (TCU) would like to inform the general public that Tanzania Business School
has invited applications including for postgraduate degrees at locations in Arusha and Dar-es-Salaam. Kindly note that the School has not been accredited to run any degree level program and those advertised are illegal and award offered will not be recognized.
The Commission has directed Tanzania Business School to immediately cease any degree level training in the country. For the non-degree programmes the Commission is advising the public to check the accreditation status of the school with National Council for Technical Education (NACTE).
Issued by:
Executive Secretary
Tanzania Commission for Universities
Mahitaji ya Kielimu hayaendani na Mgawanyiko wa muda:
ReplyDeleteTatizo hili la watu kupendelea kuhitimu kwa njia ya mkato ili kufikia malengo yao mbali mbali kama Kikazi,Kitaaluma na Kibiashara linachochewa na Mfumo mzima wa Elimu ulivyo.
Hivi jamani MAANA YA KUELIMIKA AU KUWA MSOMI NI KUTUMIA MIAKA MINGI KUVUKA VIDATO AMA KUUELEWA MTAALA HUSIKA?
KAMA VYUO NA TAASISI ZETU ZA JUU ZINGEBADILI AU KUREKEBISHA UTARATIBU HUU, NADHANI YOTE HAYA YASINGETOKEA.
1-WAPO WANAOTAFUTA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI WA KIBIASHARA, HUKU KIWANGO CHA ELIMU KIKIWA KIGEZO PIA,
2-WAPO WANAIHITAJI ELIMU KWA MALENGO YA KUKUZA UWEZO WAO NA KUPATA HADHI KATIKA BODI ZA KIBIASHARA NA UENDESHAJI,
3-WAPO WANAOTAKA KUKAMILISHA UWEZO WAO KITAALUMA KIBIASHARA,
(Hivyo walioasisi Mpango huo wa TANZANIA BUSINESS SCHOOL wamefanya utafiti mzuri wakabaini mapungufu katika mahitaji ya kielimu nchini huku wakilenga makundi hayo matatu (3) juu ya wahitaji)
KUTAHINIWA KWA MSOMI KUNATAKIWA KUZINGATIA KUUKAMILISHA MTAALA HUSIKA NA SIO KUTUMIA IDADI KUBWA YA MIAKA AKIWA MASOMONI!
Thank you TCU for this very important message. Tanzania has become Shamba la Bibi in many ways including in the Education! TCU, NACTE and other Education Authorizes; please do check the quality of even those that are accredited to offer various Certificates. It is heartening, when during recruitment, to see and find potential employees with glowing Certificate and without adequate knowledge and skills on the sector they claim to have passed exams. Save our Youth, Save our Children from the calamity of becoming MANAMBA with MBA
ReplyDeleteKazi ipo,
ReplyDeleteHuu usakaji wa Nondo za Fasta fasta ndio utakao tuumiza!
Mashariti ya Elimu ya juu yangali ni magumu wengi wanataka kusoma lakini wanshindwa kwa vikwazo hivyo.
Ndio maana Waangalizi waliopevuka wanaanzisha Saccos kama hii TANZANIA BUSINESS SCHOOL!
Watanzania,
ReplyDeleteHizi elimu za kuhitimu haraka haraka zitatupeleka pabaya!
Kinachotukwamisha ni mfumo wetu wa Kielimu usioenda na wa kati na mahitaji yetu kulingana na changamoto tuliozo nazo sasa.
Wengi wanachelea wanakuja kukuta hawakusoma wakati unafika muda wa kuona umuhimu wa elimu na ndio hapo mtu anaingia mkenge kwa kutoa pesa nyingi, asijue amekali kuti kavu?
Kumbe Taasisi ipo kizani wala haitambuliki?
Kwa upuku puku wa Taasisi za Kielimu za mikononi?
ReplyDeleteAma kweli TCU kazi mnayo!
Wajameni Tanzania tutamahitaji makubwa ya Uwekezaji katika Sekta ya Elimu kwa kuwakubalia wawekezaji wenye sifa na vigezo.
Kwa kutokana na mambo makubwa haya hapa chini:
1.KASI YA KUKUA KWA UCHUMI WETU,
Kulinga na kasi kubwa ya kukua kwa uchumi wetu inayovuka wastani wa 5% wa Dunia, Tanzania tuna 7.1% kwa mujibu wa Benki ya Dunia WB, hivyo kasi ya kukua kiuchumi inakwenda na mahitaji makubwa katika nyanja za Elimu,Utafiti na Uendelezaji (Research and Development-R&D) ,Sayansi na Teknolojia.
2.ONGEZEKO LA RIKA LA KATI LENYE UWEZO (Growing middle class),
Dunia ina taswira ya aina hii ya muundo katika idadi ya watu, hasa kwenye maeneo ambayo yana kas kubwa ya maendeleo na mahitaji ya kibiashara kama ilivyo Afrika, Afrika ya Mashariki na hasa Tanzania, hivyo Rika hili linahitaji zaidi Elimu ili kujikimu katika maisha kama yalivyo mahitaji mengine.
3.KUPATIKANA KWA RASILIMALI:
Kutokana na upatikanaji wa Rasilimali kama Madini, na vyanzo vya nishati kama Urani, Gesi na Mafuta, ndio vimekuwa vichecheo vya No.1 hapo juu yaani (KUKUA KWA KASI KWA UCHUMI)
HIVYO TCU LICHA YA KAZI KUBWA MNAYOIFANYA YA KUSIMAMIA NA KURATIBU AINA YA TAASISI ZINAZOKUBALIKA, MNAHITAJIKA ZAIDI MUAKISI NA KUSHAWISHI UWEZEKANO WA UWEPO WA WAWEKEZAJI WENGI WENYE VIGEZO VINAVYOKUBALIKA KATIKA SEKTA YA ELIMU, UTAFITI NA UENDELEZAJI, SAYANSI NA TEKNOLOJIA, ILI KWENDA NA MAHITAJI HAYO HAPO JUU MATATU (3).
Bongo Tambarale!
ReplyDeleteKatika hali ya kushangaza niliwahi kushuhudia mara kwa mara, MHADHIRI ANATOA UKUFUNZI AKIWA KATIKA MGAHAWA NA WAHITIMU WANAPATIWA STASHAHADA ZAO BAADA YA MIEZI KADHAA YA MASOMO HAPO HAPO KWENYE MGAHAWA!
Ama kweli ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni.
Unakuta Mhadhiri anatembea na Lecture notices katika sanduku la makabrasha(Brief case),mikononi na makwapani.
Wafundishwaji jukumu lao ni kufika katika Mgahawa kila siku wakiwa na note book zao na Vitabu na makaratasi ya Assignments, wakifika kila mmoja analo jukumu la KUJINUNULIA KINYWAJI YEYE MWENYEWE ILI AWEZE KUPOKEA MAFUNZO KUTOKA KWA PROFESA!.
Sasa basi, ikitokea umekuja siku huko vizuri, utakaa ukikodoa macho hata maji ya chupa huna mezani, huku ukipokea Mafunzo kavukavu hadi muda wa kuondoka, ukishuhudia wenzako wakinywa na kutafuna!
Hiyo ndiyo Trela kamili ya Ukufunzi kwenye Taasisi za ndani ya Migahawa ambazo zinatoa STASHAHADA (DEGREE) KAMILI KWA WAHITIMU Jijini Darisalama!
Je, TCU mmesha fanya ufuatiliaji huu?
Hapa ndio ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni!
Bongo Tambarale!
Tukimbilie wapi wajameni?
ReplyDeleteKiza kimetanda, tumeshikwa kote kote!
Ukienda huku kutafuta TIN ufungue biashara ujiwezeshe mwenyewe bila kuajiriwa unakutana na Vishoka!
Ukija kwenye Elimu ohhh, unakutana na Tanzania Business School!
Enhe TCU,
ReplyDeleteNa wale Maprofesa wetu tunaowaona kwenye Migahawa unamkuta Mkufunzi na chupa la maji ya Uhai ama Soda, ama Glasi ya Juisi mezani.
Ni ajabu ukitambulishwa kwake anakusajili na hapo hapo Mgahawani masomo yanaanza!
Vipi kwa nini tusianzie kwao?,
Halafu ndio tuje kwenye Taasisi zao?,
Inawezekana ni hao hao Maprofesa wa Migahawa, wanapoona wafurukute wanaamua kuanzisha Vyuo uchwara!
TCU bado mna kazi kubwa sana na bahati mbaya mfumo wetu wa wanafunzi kusoma kwa kuwindana na kubembeleza maprofesa hawasemi mengi. Vyuo vingi vinavyotoa post graduate degree wanafunzi hawamalizi kwa muda. Maprofesa wako bize nadhani ni pamoja na hizi shule nyingine za migahawani. Mimi ninakusudia kulifuatilia suala hili na nitaomba ushirikiano wenu siku si nyingi. Lakini mpaka wakati huo jee mnautaratibu gani wa kufuatilia vyuo vya uma vinavyotoa shahada za juu?
ReplyDelete