TUNAHITAJI WAHUDUMU WA OFISI WAWILI
WAWE NA UWEZO WA KUMIA COMPUTER
WAWE WANAONGEA KIINGEREZA VIZURI
KAZI ZINGINE UTAFUNDISHWA
KAZI ZAKO ZITAKUWA NI KUPOKEA SIMU NA KUFANYA BOOKINGS
TAFADHALI TUMA MAOMBI OFISINI KWETU AU TUPIGIE SIMU KWA NAMBA HIZI HAPO CHINI
TELL 01375855917
MOBILE 07903828119
FAX 01708202477
ULIZA CHRIS
"SERENGETI" THE PRIDE OF AFRICA!
Mabosi wa Serengeti Shikamoo!
ReplyDeleteJe, mimi nipo Bongo sipo huko UK na sifa zote hizo ninazo na za ziada, mfano
1-Naweza kucheza namba mbili kwa mpigo kama Juma Mkambi zaidi ya kujua Computer kama mimi ndiye Bill Gates na hicho Kiingereza mimi nafahamu hadi Romansch yaani Kiingerza cha Kizamani, ninaweza kuwa hadi Watch man wenu hapo nikimaliza kazi za Makoti makoti na matai Mchana navaa Makoti marefu ya Ulinzi na Rungu mkononi kwa Ulinzi wa Usiku.
2-Majuu kuna baridi sana, zaidi ya Ukarani wa Komputa, nitakuwa pia Mpishi wa chai za Ofisini kwa wafanyakazi na Wageni.
3-Nitakuwa pia Komedi wa kuwafurahisha Mabosi, Wafanyakazi na Wageni wa biashara hapo ambao ni Wateja (Waelezeni wazungu huko UK ya kuwa Tanzania tuna utajiri mkubwa sana wa vingi ikiwemo Komedi!!!).
Kama mtaniombea Viza nipo tayari kuja UK kikazi kukabiliana na baridi la majuu, nitaondoka Bongo huku kwenye ndege nikiwa na gunia langu la mkaa ,jiko la mkaa na pasi mkaa, ni kuwa jiko litakuwa sehemu ya kazi likinipa joto dhidi ya baridi la Majuu, wakati pasi ya mkaa itakuwa ni kama Simu ya mkononi yaani itakuwa inanipa joto nikiwa Mobile (yaani kwenye move za huko na huku) mkono mmoja simu ya mkononi na wa pili ni pasi ya mkaa (Hiyo ni akili ya jicho la tatu)!!!
Ahsanteni, naomba mnifikirie kwa Kazi hiyo!
Mimi naitaka lakini niifanyie nyumbani (work from home), vipi itawezekana.
ReplyDeleteWewe muomba kazi wa kwanza uliyepo Tanzania isije ikawa Serengeti wazee wa kazi UK wanakuombea visa unakuja UK ukifika unawageuka unakula kona unawatoroka na kuhama kabisa kwao kwenda Mtaani kubeba Maboksi!
ReplyDeleteWahindi huwa wanasea ''jumaaa wewe nakuja kuomba kaji(kazi) Kono(mikono) nyuma!,,,chacha(sasa) napata kaji(kazi) kono(mikono) bele(mbele)!''
Wabongo si tunawajua zenu za uki geu geu?