Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia Mhe. Januari Makamba 

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Serikali imeanza mchakato wa kumiliki Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa asilimia 100  ikiwa ni njia mojawapo ya kufanya mageuzi ya kibiashara na kuliendesha shirika hilo kisayansi zaidi ya ilivyo sasa.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. Januari Makamba aliyasema hayo mkoani Dodoma mwanzoni mwa wiki hii wakati akielezea mikakati mbalimbali inayotaka kuchukuliwa na serikali ili kuweza kulimiliki shirika hilo kwa asilimia 100 badala ya 65 za sasa.
Kwa sasa TTCL inamilikiwa kwa ubia, serikali ikiwa na asilimia 65 wakati 35 zinamilikiwa na kampuni ya simu za mikononi ya Airtel.
“Mazungumzo tayari yameshaanza na dhamira yetu ni kununua aslimia 35 ya hisa zinazomilikiwa na wenzetu ili serikali iweze kumiliki asilimia 100,” alisema Mh. Makamba.
Alisema katika kufanya mipango ya kwenda mbele kimaendeleo kupitia shirika hili ni lazima kufanya mchakato wa kulimiliki kwa asilimia 100 ili serikali iweze kufanya mageuzi kwa utashi wake kadiri inavyofaa.
Alifafanua kwamba hatua hii ni Kutokana na changamoto zilizopo za kimuundo, kiungozi na ndio maana serikali imechukua hatua za kinidhamu miongoni mwa baadhi ya watendaji waliobainika kutumia madaraka yao vibaya ikiwa ni pamoja na kufanya ubadhirifu na hivyo kulisababishia shirika hasara.
“Hii ni moja ya hatua muhimu katika kuelekea kufanya mageuzi katika shirika hili kongwe hapa nchini,” alisema.
Alizitaja changamoto nyingine kuwa ni matatizo ya mtaji, na kusema kuwa ni lazima yashughulikiwe ikiwa ni pamoja na kwenda na teknolojia mpya na kulifanya shirika lijiwekeze kibiashara zaidi ya ilivyo sasa.
“Naamini katika kufanya mageuzi makubwa bodi itachukua nafasi yake kwa maana ya uongozi wa shirika katika kurekebisha mambo na mapungufu yaliyopo, kwa maana ya kuweka uongozi mpya utakaoleta mabadiliko ili kulibadilisha liwe shirika kubwa la kisasa linalotengeneza faida,” alisisitiza.
Alisema kutokana na historia yake huko nyuma kampuni hii ilipaswa kuwa ndio kampuni inayoongoza kimapato na pia kwa kutoa huduma nchi nzima kutokana na kuwa ipo kila wilaya katika nchi, lakini kutokana na changamoto mbalimbali imekuwa ni tofauti na matarajio yaliyowekwa wakati huo.
Alisisitiza kuwa wakati sasa umefika kwa shirika kuwa katika mtazamo wa kuwekeza kibiashara zaidi na ushindani.
“Shirika hili kongwe limeendelea kubaki kama lilivyo na serikali imeliona hilo, kinachohitajika ni kuwekeza katika rasilimali fedha na watu ili kukabiliana na ushindani wa kibiashara uliopo sasa,” aliongeza.
Alisema mbali na changamoto zote hizo lakini TTCL imefanikiwa kuunganisha Ofisi za Serikali, mashirika mbalimbali, Taasisi za kifedha, utangazaji na Taasisi za elimu na hivyo kuboresha matumizi ya huduma za mtandao wa mawasiliano kupitia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi.

“Kwa mfano huduma za video conferencing zinawezesha kuendesha mafunzo au mikutano kwa wahusika na hivyo kuongeza ushiriki, na kupunguza gharama,” alisema.

 Akisikiliza kero za wafanyakazi wa kampuni hiyo hivi karibuni, waziri Makamba aliiagiza bodi ya Wakurugenzi ya TTCL kumtumia Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kufanya ukaguzi wa mahesabu ili kuthibitisha tuhuma za ubadhirifu wa fedha za kampuni hiyo ili hatua za kisheria wakibainika.
Baadhi ya malalamiko yaliyotolewa na wafanyakazi hao ni pamoja na uongozi na bodi dhaifu katika ufuatiliaji mambo, ubadhirifu wa fedha za kampuni pamoja na uhamisho wa wafanyakazi usofuata taratibu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Tunaitaji mapinduzi ya kweli ktk shirika hili kongwe zisijekuwa ni siasa tu hizi


    ReplyDelete
  2. TTCL ilikuwa inamilikiwa na serikali kwa asilimia 100 sababu zilizofanya hisa kuuzwa kwa wawekezaji wengine ndio hizo hizo zilizotajwa ikiwemo mtaji na tejnolojia mpya. je serekali ikizirudisha hizo hisa hayo matatizo yatapata jawabu?

    ReplyDelete
  3. HONGERA MHE. MAKAMBA HONGERA SERIKALI!!!

    Mdau wa Kwanza No.1 na wa Tatu No.3

    HUU UAMUZI UMEKUWA WAKATI MUAFAKA KABISA!

    Kwa sasa TTCL inayo nafasi kubwa saana ya kujimudu kuliko ilivyokuwa kabla.

    1.TEKNOLOJIA:
    Mkonga wa Taifa ndio huo mkononi huku Serikali ikiwa ndio Mmiliki wake. NICTBB (National Information Transmission Back Bone),,,wiki chache zilizopita TCRA ilitangaza kushusha gharama za Mawasiliano kwa Mitandao yote nchini, hivyo GHARAMA ZA MAWASILIANO ZITAKUWA NI CHINI SANA KULIKOILIVYO KUWA KABLA NA KUTOA UWEZEKANO WA SHIRIKA KUENDESHA KWA FAIDA ZAIDI.

    2.MTAJI:
    Serikali inao uwezo kwa sasa kuupata Mtaji hata kwa njia za kutoka kwenye Kianzo cha Wawekezaji wa ndani kwa kuwa Masoko ya Hisa yameimarika zaidi nchini kufuatia Uwekezaji kukua baada ya mali kupatikana nchini Gas na Madini MITAJI YA NJE INA MIMINIKA NA YA NDANI INAWEZA KUPATIAKANA HATA KAMA SIO TANZANIA KWA NCHI ZA ENEO LETU LA AFRIKA YA MASHARIKI.

    3.ICT 4 eGovernment.
    Pana mahitaji makubwa sasa kwa Serikali kufikika kwa njia ya Mtandao huku uwezekano huo ukiwepo sasa tena kwa gharama nafuu kupitia Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa, kama mlivyosikia jana Mkaguzi MKUU WA MAHESABU YA SERIKALI (ACG) AMEKWIHSHA INGIZA UTENDAJI KWENYE MKONGO WA TAIFA huku IDARA NA TAASISI ZINGINE ZA SERIKALI ZIKIFUATIA.

    INATAKIWA IFIKIE KWA KUTUMIA TTCL kwa kupitia gari (vehicle) la NICTBB uweze:- K

    -Kuomba na kutoa Passport yako Ukiwa Mbagala Rangi 3 badala ya kufika Makao Makuu ya Uhamiaji Kurasini,

    -Uweze kusoma Taarifa za Mahesabu ya Serikali ukiwa nyumbani kwako Kimara Bonyokwa Badala ya kuja Ofisi ya Mkaguzi wa Mahesabu ya Serikali (ACG) na kuomba Makabrasha ya Taarifa hizo.

    -Kwa ujumla wewe Mwananchi utaweza kuifikia Serikali ba pia Serikali kukufikia wewe kwa ufanisi kuliko ilivyokuwa hapo kabla.,,,HUKU SERIKALI IKIFANYA UFANISI MKUBWA ZAIDI NA KULETA MAENDELEO NCHINI.

    NI WAZI SERIKALI SASA ITAMUDU KULIENDESHA SHIRIKA TTCL KWA FAIDA KULIKO ILIVYOKUWA AWALI.

    Hivyo Uamuzi huu ni sahihi sana!

    ReplyDelete
  4. Hongera Serikali!

    Tunasubiri TTCL ituwezeshe zaidi na kukabiliana na Ushindani na Makampuni ya Mitandao ya Simu za Mikononi.

    ReplyDelete
  5. Hongera Serikali!

    Tunasubiri TTCL ituwezeshe zaidi na kukabiliana na Ushindani na Makampuni ya Mitandao ya Simu za Mikononi.

    ReplyDelete
  6. TTCL serikali ina hisa nyingi lakini bei ya broadband ni kubwa kuliko ughaibuni!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...