Mzee Alex Kombe
Enzi ya uhai wake

Ndugu zangu Watanzania na wengine wote.  Ni zaidi tu ya siku arobaini tangu mzee wetu Alex Kombe atutoke kwenda kwenye mapumziko ya daima.  Kwa niaba ya familia yangu, ndugu zangu na jamaa zangu na marafiki, napenda kuchukuwa fursa hii kuwashukuru wote wale ambao walishiriki kwa hali na mali kuomboleza, kutufariji, kuwa nasi siku zile zote za kusubirisha mipango ya kumsafirisha marehemu na kuhakikisha Alex anasafirishwa hadi Tanzania ambako alizikwa nyumbani kwake Kilema, Moshi.  Mazishi yake yalihudhuriwa na halaiki ya watu kutoka sehemu mbali mbali.
Familia ingependa kumshukuru kila mtu binafsi lakini haitaweza kufanya hivyo bali shukrani kwa wote, na hasa asante zetu kwa padre Evod Shao wa Kanisa Katoliki la St. Edwards, Baltimore;  Padre Callist Nyambo wa Kanisa Katoliki la All Saints, Florida, na Wachungaji wote wa The Way of the Cross Gospel Ministries, College Park, Maryland kwa kumuhudumia kiroho marehemu akiwa mgonjwa na baada ya kufariki. Shukrani maalumu ziende kwa wahudumu wote wa Kanisa Katoliki  la St. Camillus, Silver Spring, Maryland;  kwa Rais wa Jumuia ya Watanzania DMV bwana Iddi Sandaly kwa msaada wake usio na kifani wa kuwezesha marehemu kusafirishwa hadi Tanzania.  Shukrani pia kwa Balozi na maafisa wote wa Ubalozi wa Tanzania Marekani kwa misaada yao.  Bila ya kuwasahau woote wale ambao walisaidia upande wa vyakula,  vinywaji na wale waliosaidia kumhudumia wakati wa matibabu.
 Mimi na familia nzima tungependa kuwakaribisha  wote katika sala ya kumuombea na kumkumbuka ndugu yetu Alex  ambayo itafuatiwa na chakula cha mchana saa 7 mchana (1:00 pm sharp)  Jumapili Februari 17 katika kanisa la:
The Way of the Cross Gospel Ministries, 3621 Campus Drive, University of Maryland College Park, Maryland 20740.
Asante na karibuni sana,

Mrs. Mary Kombe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...