Marehemu Mzee Wilfred Mahendeka Mtaki
Ndugu Sospeter E
Mtaki wa Kimara King’ong’o jijini Dar es Salaam, anasikitika kuwatangazia kifo
cha baba yake Mzazi, Mzee Wilfred Mahendeka Mtaki kilichotokea Jumatatu,
Februari 11, 2013 jijini Dar es Salaam.
Mipango ya Mazishi
inafanyika Nyumbani kwa mtoto wa Marehemu Kimara King’ong’o. Misa ya kumwombea Marehemu
itafanyika Alhamisi Februari 14 kuanzia saa 5 asubuhi Katika Kanisa la Mt.
Marie Clare Michungwani.
Heshima za mwisho
zitaanza saa 7 mchana na baade safari ya kuelekea kijijini kwake
Kisorya-wilayani Bunda itaanza.
Bwana Alioa na Bwana
ametwaa- Jina lake Lihimidiwe.
Nilisoma na mtu mmoja sengerema sekondari ,anaitwa Magayane Mahendeka je mzee huyu ndiye mzazi wake?
ReplyDeleteR.I.P, Kiungwana kwanza unaanza na pole kisha ndio uanze kumuulizia skuli mate wako.
ReplyDeletePoleni sana wanafamilia. Mwenyezi Mungu awape nguvu na moyo wa kupokea na kuuchukua msiba huu kwa imani kuu. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake na lihimidiwe, Amen.
ReplyDeleteDr. Primus
RIP ....
ReplyDeletePrimus naona ilibidi uweke Dr. kwa mbele kabisa