WIMBI la wizi wa kompyuta kwenye magari sasa limeshika kasi na wezi hao wamekuwa wakibadili mbinu kila kukicha.

Gari linaloonekana hapo limevunjwa kioo kwa namna yake na wezi hao waliokuwa katika gari aina ya Harrier ya Silver walifanikiwa kuchukua vilivyomo kwenye gari ikiwemo kompyuta ndogo maarufu kamakompyuta mpakato.

Tukio hilo limetokea leo majira ya saa nane mchana karibu na kituo cha mafuta cha Victoria.

Watu hao walikuja na kupaki gari karibu kabisa na gari hilo na wala huwezi kudhani kwamba wana nia mbaya kumbe hupulizia aina Fulani ya madawa ambayo hayajafahamika na kioo hupukutika hapo hapo.

Kitendo cha wizi huo kilifanyika ndani ya dakika moja au mbili kwani mwenye gari alikuwa jirani kabisa na gari lake na aliliona gari hilo likiwa karibu ila hakuwa na wasiwasi juu la jambo lolote lile.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Mnaotembea na Laptop kwenye magari,hata kama ni kushuka mita 2 kutoka kwenye gari lako shuka na Laptop yako.Mimi Dar huwa naacha mihela kibao kwenye gari,hawachukui,wanataka LAPTOP!

    Hiyo dawa ya kupasua vioo siyo issue sana,wakati dada zetu wanachangamkia kubadili nywele zao nzuri za asilia walikuwa wanatumia dawa fulani('karikti') basi zile nywele zenye dawa ile zilipokuwa zinagusa kioo cha gari,kioo kinapasuka(nilisikia,sikuwahi kushuhudia),could be the same chemical/chemical composition.

    David V

    ReplyDelete
  2. Mie huwa nashaanga ivi mpaka leo iwe haijulikani ni dawa gani inayotumika kulainisha na kuvunja vioo vya magari? ivi kweli tunavitengo vilivyokamilika vyenye kujua wajibu wao?mbona ni kazi rahisi sana?nina hakika kuwa zinazotumika ni kemikali sasa ni kweli nchi nzima haina mtaalamu wa kulifuatilia hili suala na kugundua ni kemikali gani kisha itoe jawabu au ufumbuzi wa tatizo hili?Ni wazi kwamba kemikali inayotumika ikigundulika basi utakua mwanzo wa kupambambana na hili tatizo kwakua itafuatiliwa wapi inapopatikana na nani huwa anatoa kwa misingi ipi?vinginevyo labda kuwe na ushirikiano na hao wezi.

    ReplyDelete

  3. Ishh Jamani mbona huo wizi sio mpya kabisaaa ni mara ngapi watu wamelalamika kwamba wanaibiwa laptop kwenye gari aina hyo watu wanatakiwa kuweka laptop chini ya kiti ama washuke nayo

    huyu mtu hata aitaji pole ni uzembe wake kwani huo wizi uko kia mahali sio dar peke yake hata ukiwa bali, Indonesia kuna case kama hizo
    ukiwa Johor, Malaysia the same thing watu wanashuka na vitu vyao au wanaweka mahali ambapo havita onekana ili kumvutia mwizi

    ReplyDelete
  4. Pole sana,
    Lakini angalia sana kuweka vitu vyenye dhamani ndani ya gari lako,
    kama unataka kutoka bora utoke navyo au acha mtu kwenye gari lako.

    ReplyDelete
  5. Harrier rangi ya Silver mnaendesha lakini Mipango ya Maisha Mjini hamna,,,mnategemea wizi!

    Hii ndio taswira ya hali halisi, siku hizi usifikiri mtu kuwa na gari ndio mambo yake safi NO!

    ReplyDelete
  6. we ndo umejua leo mbona ipo siku mingi iyo ndugu

    ReplyDelete
  7. DIGITAL....................
    TUTAKOMA WALAAH HII TECNOLOGIA SII MCHEZO DUH WE HAVE TO TAKE ACTION SOON.

    ReplyDelete
  8. Wanatumia mafuta ya curl (ya kina mama). Sasa jiulize kama yanabomoa kioo ndani ya dakika 2 je humo vichwani mwa kina mama panaharibika kiasi gani? Ndio maana tunapewa majibu ya mkato mkato na mepesi mepesi tu siku hizi. Na ndio maana ndoa imekuwa ndoano.

    ReplyDelete
  9. Hiyo ni changamoto kwa Ukosefu wa Ajira nchini.

    Hivi mtu unamudu kuendesha Harrier halafu unakuwa mwizi, tena sio mwizi Mheshimiwa kama waleee mwizi mwizi mbwa?

    Kwa nini kama mambo yamekataa usiwashe Harrier yako uende Sokoni Kariakoo Alfajiri na Gunia lako tupu kwenye buti la gari, ukifika uombe mzigo mali kauli kwa Madalali wa mboga utandike gunia lako chini upange mafungu ya mboga Bamia, nyanya chungu na kunde mbichi uuze, ?

    Wewe unakaa Mwenge nani atakujua Kariakoo?

    Akija mtu anayekujua itabidi uwe kauzu umwambie nipo katika Ekting ya Sinema ni Mchezo wa Picha nacheza tu,,,wala sipo kwenye biashara kumbe Mzee mzima unaua Kenge kiufundi!!!

    Si utapata tu kama riziki za kaiwada?

    Kazi ni kazi bora iwe halali na mkono wende kinywani Mwanawane!

    ReplyDelete
  10. Ohhh Bongo tambarale!

    Wewe mwenye harrier unaiba kwa kuvunja, sasa mwendesha Baiskeli si ndio ataiba Soketi ukutani, swichi na kun'goa na waya zake ukutani kabisa?

    ReplyDelete
  11. Sasa tutaweka grill kwenye magari yetu mfano wa magari ya kivita!!

    ReplyDelete
  12. VIPAUMBELE VYA KIMAISHA:

    1.GARI (HARRIER)
    2.CHAKULA
    3.MAHALI PA KULALA
    4.MAVAZI
    5.MATIBABU
    6.ELIMU KWA WATOTO
    7.POMBE NA NYUMBA NDOGO(Baadhi ya watu)
    8.AKIBA YA ZIADA(Guta,Toyo,Bajaj,Mkokoteni,Genge la Bamia na Dagaa)
    9.DIRA YA MAISHA
    10.HATMA YA BAADAYE YA MAISHA


    Sasa bosi Mwizi unayetumia gari zuri kabisa aina ya Harrier, MAISHA YANA VIPAUMBELE (KWA MPANGILIO WA KUANZIA CHA JUU ZAIDI) KATIKA VILE UWEZO ULIONAO NA MACHAGUZI YA MAHITAJI KAMA HAYO HAPO KUMI (10) JUU KWA UCHACHE.

    SASA KWA NINI BADALA YA KUNUNUA HIYO HARRIER USINGECHAGUA NO.8 UKAPATA ,,,8.AKIBA YA ZIADA(Guta,Toyo,Bajaj,Mkokoteni,Genge la Bamia na Dagaa),,,KWA UHAKIKA ZAIDI WA MAISHA YAKO NA KUTUWA KWA MOYO BADALA YA KUJIPA PRESHA KWA KUCHAGUA MAISHA GHALI (KUWA NA HARRIER) WAKATI HUNA KAZI YA UHAKIKA AMBAYO YANAKUSUKUMA SASA UNAKUWA MWIZI?

    ReplyDelete
  13. Harrie mmeishusha thamani jamani!

    Wenye Harrier badilisheni usafiri nunueni BAJAJ na TOYO ama MAGUTA, ni vile heshima ya gari aina hiyo imeshuka, aina hiyo ya gari imetumiwa na wezi!

    ReplyDelete
  14. Dawa ni kualika Makampuni ya kufunga 'surveillance cameras' kwenye magari.

    Hapo ndio tutashuhudia watu wanaoheshimika ktk jamii wakinyata kuvunja na kuiba ndani ya magari!

    ReplyDelete
  15. Ole wao waliokumbuka rangi ya gari wakasahau namba yake (jamaa amekumbuka harrier ya silver, namba haijui, nadhani kuna haja kila gari inayokusogelea katika mazingira ya utata unai-note namba yake

    ReplyDelete

  16. Shuka na vitu vyako vya THAMANI tafadhali, wawe wanaambulia power window switches na ushuzi mwingine sio important items like your STORED DATA.

    ReplyDelete
  17. KWA NINI MSIRUDISHE MPIRA KWA KIPA?

    Mambo yakikataa Mijini ni vema kwa busara turudi Vijijini makwetu (KURUDISHA MPIRA KWA KIPA) tukalime badala ya kufanya Wizi utakao tugharimu na kutuaibisha tuking'ang'ania kukaa Mijini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...