CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimefuta wazo la kuendesha mdahalo kwa wagombea wa nafasi za juu za uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Mdahalo huo ulikuwa ufanyike Februari 15, 2013 na tayari chama kilikuwa katika hatua nzuri ya mazungumzo na wadhamini pamoja na kituo kimoja cha televisheni kwa ajili ya kurusha 'live' tukio hilo, ambapo kesho ilikuwa tutangaze utaratibu mzima wa mdahalo huo.

Katika mazungumzo ya leo na uongozi wa kituo hicho ambao hautaki tukitangaze, tumekubaliana kufuta wazo la mdahalo kwa sababu nafasi ya urais amebaki mgombea mmoja, hivyo mdahalo hautakuwa na tija.

Dhamira ya awali ya kufanya mdahalo ilikuwa kuwapa fursa wapiga kura wasikie vyema sera za wagombea urais na Makamu wa Rais, ili wananchi wawasikilize wagombea hao na pia wapiga kura wawatambue vizuri.

Hata hivyo TASWA itatafuta utaratibu mwingine mzuri ambao utawezesha wagombea kuzungumza na waandishi wa habari na kuulizwa maswali mbalimbali ambayo tunaamini kwa kiasi fulani yatasaidia wapiga kura katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Februari 24 mwaka huu. TASWA inawatakia kila la kheri wagombea wote wa TFF waliobakia.

TASWA imekuwa ikifanya mdahalo kwa wagombea wa nafasi za juu kwenye uchaguzi wa TFF, ilifanya hivyo mwaka 2001 na mwaka 2004 ingawa haukuwa wa live, ikafanya wa live mwaka 2008, ambapo yote ilikuwa ya mafanikio makubwa.

Nawasilisha.
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. KWA NINI MDAHALO UFUTWE?

    HATA KAMA WAGOMBEA NI MMOJA MFANO KWA NGAZI YA URAISI?

    Wagombea Uongozi ngazi za juu, palikuwa na kila sababu mdahalo uendeshwe tena ingebidi kwa njia ya Televisheni ili wananchi waweze kuona Wananchi na kuwauliza maswali na kupata Mgombea anayekubalika zaidi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...