Miss Utalii Tanzania 2012/13 wiki ijayo wataanza ziara ndefu ya kutembelea Hifadhi za Taifa na vivutio vya utalii katika mikoa ya Dar es salaam,Morogoro,Mtwara,Lindi na Pwani.

 Vivutio hivyo ni pamoja na Hifadhi za Taifa za Mikumi, Udizungwa, Saadani, Selous, pia maeneo ya kihistoria ya Bagamoyo, Amboni, Kijiji cha makumbusho,Makumbusho ya Taifa, Pugu sekondari,maeneo mengine ni ufukwe wa kigamboni, soko la kimataifa la magogoni, uwanja wa taifa, Julius Nyerere International Airport, Soko la kariakoo, mashule ya sekondari na msingi, pia watatembelea manispaa za ilala, temeke na kinondoni ambapo watakutana na viongozi wakuu wa wilaya, mikoa, na wabunge katika majimbo ya mikoa hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Sisi kaka/baba/wajomba zenu ,n.k tunawapenda sana na tungependelea zaidi,kama inawezekana, mvae kama mlivyovaa hapo kwenye picha ya kwanza juu.Ona Mnavyopendeza sasa!Nadhani nimeeleweka ninachotaka kueleza.Aliyebuni mavazi hayo nampa 5(Hapa naweza kuambiwa nini bwana wewe David V,watu wanakwenda na WAKATI,n.k)

    David V

    ReplyDelete
  2. Kweli hiyo picha ya kwanza mnapendeza sana Malaika wetu na nguo zenu za Kiafrika. Nawapa pongezi sana kwa uzuri.

    ReplyDelete
  3. Kweli picha ya kwanza Mswanoooooooo hebu nasi Tanzaania tuwe tufauti na wao watuige kwa vazi la picha za juu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...